Ikiwa imebaki Siku Moja kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewakumbusha na kuwahimiza watumishi wa Umma Mkoa wa Lindi kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025 ikiwa ni haki ya kikatiba kwa kila mwananchi. Wito huo ameutoa Oktoba 27, 2025 katika kikao chake cha kawaida cha kiutendaji kilichofanyika katika ukumbi Mkubwa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi. Amesema, watumishi wa umma ni mabalozi wazuri kwa jamii hivyo ni vema kuonesha mfano kwa vitendo ikiwemo kujitokeza mapema kupiga kura kwa kuwa ni haki ya msingi kufanya hivyo. Wito huo umekuja ikiwa imebaki siku moja kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Tanzania. Huku kauli mbiu ya uchaguzi ikisema “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.