Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi eneo la utawala Ndugu Nathalis Linuma amewataka watumishi wa umma kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kuchukua hatua za haraka katika kujilinda na magonjwa yanayoambukiza na yasiyo ambaukiza .
Wito huo ameutoa alipokuwa anazungumza na watumishi kwaniaba ya katibu Tawala Mkoa katika ukumbi Mkubwa wa ofisi za Mkuu wa Mkoa .
"Utaratibu unatutaka kufanya vikao vinavyohusu elimu ya afya na upimaji mara mbili kwa mwaka lengo kukumbushana wajibu wa kulinda afya zetu na kuendelea kuchukua tahadhari zidi ya magonjwa nyemelezi. Inafahamika kuwa mtumishi anapokuwa na afya njema anaweza kufanya kazi kwa zaidi lakini hata ambaye anagundulika anachangamoto za kiafya ni rahisi kupangiwa majukumu kulingana na changamoto yake na kupata haki zake za msingi " Amesema Linuma .
Watumishi wamepata elimu ya lishe, Afya ya akili, magonjwa yanayoambukiza na yasiyo ambukiza pamoja na elimu kutoka TAKUKURU.
@wizara_afyatz
@ortamisemi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.