Mgeni Rasmi wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani Dkt Enock Chilumba akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa kwaniaba ya katibu Tawala Mkoa, amewakumbusha wauguzi kuhakikisha wanazingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi ya lugha nzuri kwa wagonjwa.
Dkt. Chilumba ametoa wito huo tarehe 13 juni 2025 katika viwanja vya sokoni vilivyopo kata ya Majengo Halmashauri ya Mtama.
“Wauguzi mnatakiwa kuhakikisha mnatoa huduma za afya zinazozingatia ubora wa kazi zenu ikiwa ni pamoja na kuzingatia utu, stara na lugha njema kwa wagonjwa lakini pia mnapaswa kuzingatia miongozo mbalimbali ya Serikali na taaluma yenu ili kuweza kukidhi ubora wa huduma mnazozitoa’’ alisema Dkt. Chilumba.
Awali, Damasiana Msala kwaniaba ya wauguzi, amesema kuwa licha ya changamoto mbalimbali ambazo zipo, i wameahidi kuendelea kuzingatia miiko na maadili ya kazi yao na kufanya kazi kwa weledi ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassani katika harakati zote anazozifanya za kuhakikisha sekta ya Afya inakuwa bora na kimbilio la Wanaanchi.
Maadhimisho hayo meambatana na maandamano ya Amani kutoka kituo cha afya Mtama hadi viwanja vya sokoni vilivyopo kata ya majengo.
Katika kudymisha upendo na uhusiano nzuri na jamii, wauguzi wamefanya matendo ya huruma kwa kutoa mahitaji mbalimbali kama vile sabuni kwa wagonjwa waliopo katika wodi ya watoto na watu wazima ndani ya kituo cha afya Mtama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.