Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo ameendesha hafla fupi ya utowaji mikopo ya 10% ya mapato ya Halmashauri kwa vikundi vya Wanawake, Vjana na Watu wenye ulemavu, mikopo hiyo ni Shilingi Milioni 800, zoezi hilo limefanyika katika viwanja wa Shule ya Msingi Majengo.
Mhe. Moyo amewataka viongozi wa Wilaya na Halmashauri kuhakikisha kanuni za utoaji mikopo zinazingatiwa na mikopo inasambazwa kwa haki na kwa wakati ili kutimiza lengo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Daktari Samia Suluhu Hassan ya kuwakwamua vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kutoka katika umasikini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea ndugu Joshua Mnyang'ali amesema kuwa vikundi 33 vya wanawake vimepata Shilingi Milioni 365, vikundi 22 vya vijana vimepata Milioni 375 na vikundi 5 vya walemavu vimepata Milioni 60 pia, amesisitiza kuwa usimamizi wa mikopo unahitaji juhudi za pamoja ili kuhakikisha mikopo inasambazwa vizuri na inarejeshwa kwa wakati
Nae, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhe. Adinan Mpyagila, amewasihi wanufaika kutumia mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na kurejesha kwa wakati ili watakaoomba kwa awamu zijazo waweze kupata kwa wakati.
Aidha, Wanufaika wa mikopo hiyo Hadja Saidi Ng'ombo Katibu wa kikundi cha Chikumbila Kata ya Marambo.
Brigta Andrea Mwenyekiti wa Bry Toto food point.Mfaume Hassan Namkaa Mwenyekiti Kikundi cha Amu Agro Business.
Mwenyekiti wa kikundi cha walemavu msichoke
wameishukuru serikali kwa kuwawezesha na wameahidi kurejesha mikopo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.