BIASHARA NA UWEKEZAJI
Biashara katika Mkoa inakua kwa kasi ya wastani kwani shughuli muhimu za kiuchumi Mkoani ni za kilimo pamoja na Uvuvi. Serikali imerejesha utaratibu wa kutoa leseni za biashara kwa kutoza ada kama ilivyokuwa mwaka 2004 na hivyo kuziwezesha Halmashauri zetu kujiongezea mapato ya ndani kutokana na chanzo hiki.
2.0 Wawekezaji
Katika kuhakikisha fursa za mkoa wa Lindi zinatumika ipasavyo, mkoa unaendelea kukusanya takwimu za uwekezaji kutoka halmashauri zote za mkoa wa Lindi ili kuweza kuwa na mikakati madhubuti ya uwekezaji na hadi sasa tuna takwimu za halmashauri mbili ikiwemo Nachingwea na Manispaa ya Lindi ambapo takwimu hizo zinaonyesha jumla ya wawekezaji walioko Manispaa ya Lindi ni 154 na Nachingwea ni 23, takwimu hizo zikihusisha wawekezaji wadogo na wakubwa.
Mkoa wa Lindi kama ilivyo kwa mikoa mingine inavyo viwanda vya aina tatu ambavyo ni viwanda vikubwa; vya kati na vidogo. Katika mkoa tunavyo viwanda vikubwa vitatu vya kubangua korosho ambavyo kwa sasa vyote vimefungwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mitambo. Aidha kwa kushirikisha wadau mbalimbali; juhudi zinafanywa ili viweze kufufuliwa na vifanye kazi ya kuongeza thamani ya zao la korosho, kuongeza ajira hatimae kuongeza thamani ya zao la korosho katika soko la ndani na nje. Mkoa pia una viwanda vya kati ambavyo kwa kiwango kikubwa vinajihusisha na uchakataji wa magogo na mbao katika wilaya zote tano za mkoa wetu. Hivi pia vimewezesha kupanua uwanda wa ajira kwa wakazi wa mkoa wa Lindi.
Vipo pia viwanda vidogo ambavyo kwa kiwango kikubwa vinachangia katika kutoa ajira na kuinua pato la kaya na jamii kwa ujumla. Viwanda hivi ni vile vya kusindika samaki (Kamba kochi na pweza) vilivyopo Kilwa, viwanda vidogo vya useremala, ukamuaji mafuta ya alizeti, ubanguaji mdogo wa korosho, ushonaji nguo hasa unifomu za wanafunzi,uchomeaji wa vyuma vya matumizi ya majumbani, karakana na viwandani, utengenezaji wa matofali ya ujenzi wa nyumba na barabara na usindikaji wa unga wa muhogo na viwanda hivi vinapatikana katika wilaya zote za mkoa wa Lindi.
Mkoa wa Lindi umepokea wawekezaji wengi wakubwa katika ardhi ambao uwekezaji wao una mahusiano ya karibu na ukuzaji wa viwanda. Aidha hadi kufikia mwaka 2015/2016 wawekezaji 6 wameonesha nia ya kuwekeza katika ardhi uwekezaji ambao utachangia upatikanaji wa ajira, uongezaji kipato na upunguzaji umaskini na uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata gesi asilia, madini ya risasi, na viwanda vya mihogo kama ilivyooneshwa katika jedwali na. 1
Jedwali Na. 1: Uwekezaji Katika Ardhi Ambao Shughuli Zake Zinaendelea Kwa Sasa
Na
|
Kampuni Ya Uwekezaji
|
Mahali Anapowekeza.
|
Matumizi Ya Ardhi
|
Ukubwa Wa Ardhi (Ha.)
|
Hali Halisi
|
1.
|
CASSAVA STARCH OF TANZANIA CORPORATION LT.D
|
Wilaya ya Lindi. Vijiji 6 vya Mandwanga, Linoha, Nahukahuka A na B, Lipome na Lindwandwali.
|
Kilimo cha Mihogo
|
3,004.011
|
Amekwishapata hekta1,752. Uthamini Kijiji Lipome, Lindwandwa
li na Linoha umekamilika. Fidia imelipwa kijiji cha Lipome na Lindwandwali. |
2.
|
URANEX
|
Wilaya ya Ruangwa. Vijiji sita 7 vya mradi wa machimbo ya Graphite.
|
Machimbo ya madini ya Risasi (Graphite)
|
3,013
|
Uthamini kwa ajili ya fidia umekamilika na ulipaji wa fidia unaendelea unatarajia kukamilika mwezi huu wa Januari, 2017.
|
3
|
TPDC/ MINJIGU PHOSPHATE MINING
|
Wilaya ya Kilwa. Eneo la katika Kiwanja Na. 1 Kitalu K. KILAMCO Kilwa Mjini.
|
Ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea
|
60
|
Usanifu mradi na Uthamini wa mali katika eneo hilo umekamilika.
|
4
|
M/S OYO REAL ESTATE CO. LTD
|
Wilaya ya Kilwa. Vijiji vya Mtandi na Rushungi.
|
Viwanda vya mazao ya mafuta.
|
1,426.
|
Mpango wa Matumizi ya Ardhi na uhawilishaji umekamilika
|
5
|
GREEN RESOURCES TZ. LTD.
|
Wilaya ya Lindi. Vijiji vya vine (4) Hingawali, Msangya- Navanga, Nachunyu, Simana n.k
|
Kilimo cha Miti ya mbao na utunzaji mazingira
|
2,500
|
Mpango wa Matumizi bora uko Wizara ya Ardhi kuidhinishwa.
|
6
|
STAT OIL, EXONMOBIL, OPHIR ENERGY, SHELL LTD & PAVILION, Ophir
|
Manispaa ya Lindi. Eneo la Kikwetu.
|
Ujenzi wa Mtambo wa Gesi Asilia (LNG)
|
2,071
|
Upimaji ardhi na Hatimiliki umekamilika. Uthamini umekamilika.
Fidia bado. |
5.0 Mikakati iliyowekwa kimkoa
Kutokana na mkoa wa Lindi kuwa na fursa nyingi za uwekezaji, bado mkoa unahitaji kuwa na wawekezaji wakubwa watakaoweza kuzitumia fursa hizo ipasavyo. Mikakati madhubuti ya kutangaza utajiri wa fursa za mkoa wa Lindi kwa wawekezaji wakubwa zimewekwa na zimeanza kufanyiwa kazi ya utekelezaji. mikakati hiyo ni kama ifuatayo;
Mkoa katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu kuhusu kutenga maeneo ya wafanya biashara ndogo ndogo, tayari maeneo hayo yametengwa kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 66
Jedwali Na. 2 Maeneo Yaliyotengwa Kwa Ajili Ya Biashara Ndogo Ndogo Katika Mkoa wa Lindi
Na
|
Halmashauri
|
Maeneo
|
Maelezo
|
1
|
Lindi Manispaa
|
Mwenge Saba saba Mitwero
|
Ukubwa wa maeneo yaliyotengwa ni ekari zisizopungua 5
|
2
|
Lindi
|
Mihogoni-Mtama
|
Tayari viwanja 350 vimetengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo
|
3
|
Kilwa
|
Kilwa masoko
|
Ukubwa wa maeneo yaliyotengwa ni Ekari 6.37
|
4
|
Nachingwea
|
Block F (VODA)
|
Eneo lenye uwezo wa wafanyabiashara 150
|
Uhindini Block C
|
Eneo lenye uwezo wa wafanyabiashara 80
|
||
Bondeni area
|
Eneo lenye uwezo wa wafanyabiashara 300
|
||
5
|
Ruangwa
|
Kilimahewa, Dodoma na Namakonde
|
Ukubwa wa maeneo yaliyotengwa ni ekari zisizopungua 5
|
6
|
Liwale
|
Eneo la wajasiliamali vijana na wanawake liwale
|
Ukubwa wa maeneo yaliyotengwa ni ekari zisizopungua 4
|
Eneo la soko
|
Ukubwa wa maeneo yaliyotengwa ni ekari zisizopungua 1
|
||
Eneo la viwanda vidogo (SIDO)
|
Ukubwa wa maeneo yaliyotengwa ni ekari zisizopungua 1
|
MAENEO NA FURSA KWA AJILI YA UWEKEZAJI KWA KILA HALMASHAURI KATIKA MKOA WA LINDI
Na.
|
Halmashauri
|
Eneo Liliotengwa
|
Ukubwa wa eneo (Ha)
|
Matumizi
|
Maelezo
|
1
|
Lindi MC
|
Mkwaya-Likono
|
Km 112
|
Fukwe kwa ajili ya burudani
|
Eneo la pembezoni mwa bahari ya Lindi
|
Kikwetu
|
2,071.705
|
LNG
|
limeshapimwa
|
||
|
5,000
|
Chuo Kikuu
|
Limetengwa halihitaji fidia
|
||
2
|
Lindi DC
|
Mipingo
|
322,705
|
Kilimo cha Ufuta
|
Eneo limetengwa, Halijapimwa
|
Chiponda
|
48,908
|
Ufugaji wa nyuki katika misitu
|
Eneo halijapimwa lakini halihitaji fidia
|
||
Sudi, Mchinga, Mongomongo, Shuka, Ruvu
|
Km 170
|
Hoteli na maeneo ya burudani
|
Halijapimwa, linahitaji fidia
|
||
3
|
Kilwa
|
Matandu, Bonde la Mavuji, Migurue na Lihimalyao
|
47,223
|
Kilimo
|
Eneo lina milikiwa na kijiji halijapimwa
|
Hoteli tatu, Kivinje na Kilwa Masoko
|
500
|
Viwanda
|
Eneo lina milikiwa na kijiji halijapimwa
|
||
Kilwa Kisiwani, Kilwa kivinje, Nang’oma na Selous
|
844.24
|
Utalii
|
Eneo limetengwa lakini halijapimwa
|
||
Kisiwa cha Songosongo, Kilwa Kivinje, Somanga, Kilwa Kisiwani, na Songomnara
|
1,221.52
|
Uvuvi
|
Eneo limetengwa lakini halijapimwa
|
||
Mandawa, Hoteli tatu na Mavuji
|
200
|
Madini
|
Eneo limetengwa lakini halijapimwa
|
||
4
|
Ruangwa
|
Luchelegwa, Mnacho na Makanjiro
|
127,999
|
Kilimo cha Mihogo na ufuta
|
Limepimwa na linahitaji fidia
|
Kilimahewa
|
69
|
Uwekezaji wa Majengo
|
Limepimwa na linahitaji fidia
|
||
5
|
Nachingwea
|
Bondeni Road
|
8,100
|
Viwanda
|
Limepimwa na linahitaji fidia
|
Bondeni Road
|
6,199.3
|
Majengo ya biashara
|
1,815.8Ha yamepimwa na yanahitaji fidia na yanayoendelea na upimaji 4383.5Ha
|
||
Bondeni road
|
8,348.1
|
Ujenzi wa shule
|
limepimwa na linahitaji fidia
|
||
6
|
Liwale
|
Mpirani
|
2.4
|
Viwanda vya kuchakata madini,
|
Limepimwa, linahitaji fidia
|
Kichonda, Darajani na Mihumo
|
5,387
|
Kilimo cha Muhogo
|
Limepimwa linahitaji fidia
|
||
Jumuiya ya Magingo (WMA)
|
5,700
|
Utalii/uwindaji
|
Eneo lipo na linatumika kwa makubaliano na Jumuiya
|
||
Msitu wa Angai
|
139,420
|
Uvunaji wa mbao na asali
|
Makubaliano na vijiji kwa ajili ya uvunaji
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.