Adv. Mariam Kashule
Kaimu Mkuu wa Kitengo - Sheria
Kitengo cha huduma za sheria ndio muhimili mkuu katika masuala yote yanayohusu sheria katika Sekretariati ya Mkoa.
Majukumu ya Kitengo
1.Kutoa ushauri na usaidizi wa kisheria kwa Sekretariati ya Mkoa katika kutafasiri sheria, mikataba ya aina zote ambapo Sekretariati ya Mkoa ni sehemu, makubaliano ya kiushirikiano na nyaraka nyingine zote ikiwa ni pamoja na, kuwa kiunganishi kati ya Sekretariati Mkoa na Mkurugenzi wa huduma za Sheria OR-TAMISEMI na Ofisi ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
2.Kushiriki katika mikutano na majadiliano ambayo yanahihitaji au hushirikisha ushauri wa kisheria kwa ushirikiano na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria OR-TAMISEMI na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
3.Kutafasiri sheria na miongozo kwa niaba ya Sekretariati ya Mkoa kwa ushirikiano na mashauriano na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria OR-TAMISEMI na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
4.Kushirikiana na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria OR-TAMISEMI na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kuendesha mashauri na madai ambayo Sekretariati ya Mkoa au Halmashauri ni sehemu.
5.Kuratibu upitiaji na uboreshaji wa nyaraka mbalimbali ikiwemo mikataba, makubaliano, maagizo, miongozo na nyaraka za makabidhiano ambapo Sekretariati ya Mkoa na Halmashauri ni sehemu.
6.Kusimamia, kuratibu na kutoa maoni juu ya sheria na miongozo na kanuni zinazohusu Halmashauri.
7.Kusaidia kupitia na kutoa mapendekezo kwenye taarifa na nyaraka za Halamshauri zinazohusu au kuhusisha masuala ya kisheria pamoja na kuzijulisha mamlaka za juu pale inapobidi.
8.Kushiriki na kuwa sehemu ya badhi ya bodi za kudumu, kamati na vikosi kazi kwa ajili ya kazi maalumu.
9.Kutekeleza majukumu mengine kadiri itakavyo amriwa au elekezwa na Mwajiri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.