Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack leo Mei 03, 2025 ameendesha kikao cha Kamati ya lishe ngazi ya Mkoa kujadili taarifa za utekelezaji wa mkataba wa lishe, Programu Jumuishi ya MMMAM, chanjo na kadi viashiria vya afya na kuagiza kuanzishwa kwa mashamba darasa katika kata ambayo yatatumika na wanajamii kujifunza na kupata hamasa ya kulima mazao ya chakula kinachohitajika kwa uboreshaji wa afya zao na kupata akiba ya chakula.
Mhe. Telack pia amewataka viongozi wanaosimamia utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kutengeneza mfumo utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa ili ziwasaidie kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu lishe zinazowakabili wananchi waliopo katika maeneo yao.
Aidha, amezipongeza Halmashauri zilizopata ushindi na kutunukiwa zawadi kwa kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa lishe na viashiria na kusisitiza utengaji wa bajeti za utekelezaji wa afua za lishe ili kuweza kufikia malengo yaliyokubaliwa katika mkataba wa lishe.
Aidha, Mhe. Telack amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha vituo vilivyojengea na kupatiwa vifaa vya upasuaji kuhakikisha vituo hivyo vinaanza kutoa huduma za upasuaji sambamba na kuhakikisha kuwa vinapata huduma zote muhimu ikiwemo maji na umeme vitakavyowezesha utolewaji wa huduma hizo.
Pia, Mkuu wa Mkoa amesisitiza matumizi ya mfumo wa Got-Homis ili kuweza kudhibiti mapato yanayopatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.