Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa wazazi na wanajamii kurudi kubeba jukumu la kulea watoto wao ili kuweza kuwakuza na kuwajenga kiakili, kimaadili na kitabia zinazokubalika ndani ya jamii ili kujenga kizazi na jamii yenye maadili na mienendo inayokubalika.
Mhe. Telack ameyasema hayo baada ya kupokea utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto Tanzania (PJT-MMMAM) ambao una lengo la kuangazia na kuboresha Afya bora, lishe, malezi yenye muitikio, fursa za ujifunzaji wa awali pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto huku walengwa wake wakuu wa programu hii wakiwa ni watoto wenye umri kuanzia miaka 0-8 na wamama wajawazito.
Mkuu wa Mkoa pia amezitaka Halmashauri kufatilia vituo vya kulelea watoto maarufu kama Day care centre ili kujiridhisha na hali ya utoaji wa huduma za malezi na elimu kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka mitatu hadi mitano. Aidha, kuhakikisha kuwa watoa huduma za malezi katika vituo hivyo wamepitia programu ya mafunzo ya malezi kwa watoto wenye umri husika.
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Lindi Ndg. Meshack wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa programu ya PJT-MMMAM mkoani Lindi na kueleza kuwa katika utekelezaji wa programu hii unahusisha ushirikiano wa idara za Maendeleo ya Jamii, Elimu na Afya na kuongeza kuwa jamii inapaswa kuzingatia ubora wa taarifa zinazopokelewa na ubongo wa mtoto hususan katika kipindi cha umri wa kuanzia miaka 0-8.
"Kipindi cha ukuaji wa mtoto hushamiri zaidi katika kipindi cha umri wa miaka 0-8 kimwili,kiakili,kihisia na kijamii kupitia milango mitano ya fahamu kupitia kunusa,kusikia,kuona,kuongea na kuhisi, hivyo tunaelekezwa kuelimisha jamii kuzingatia sana taarifa zinazopokelewa na kupelekwa kwenye ubongo wa mtoto ili kuweza kumkuza kitabia na kimaadili" ameeleza Afisa Ustawi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.