TAARIFA YA HALI YA HUDUMA YA MAJI MKOANI LINDI
1.0 Utangulizi
1.1 Hali ya huduma ya Maji Mkoa wa Lindi
Sensa ya mwaka 2012 inaonesha kuwa Mkoa wa Lindi ulikuwa na wakazi wapatao 864,652, hadi kufikia mwezi Agosti, 2018 inakadiriwa jumla ya wakazi 413,503 sawa na asilimia 54.9 ya wakazi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama. Huduma hii inatolewa kwa kutumia vyanzo vya maji vikiwemo visima virefu na visima vifupi vyenye pampu za mkono, miradi ya mtandao wa bomba wa kusukuma kwa mashine, miradi ya maporomoko na uvunaji wa maji ya mvua.
1.1.1 Mpango wa Kuongeza Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini
1.1.2 Utekelezaji wa Miradi katika Vijiji 10 katika kila Halmashauri
Hadi kufikia mwezi Agosti, 2018 jumla ya miradi 39 katika Halmashauri za Mkoa wa Lindi inatekelezwa kupitia Mpango wa maendeleo sekta ya maji awamu ya I (WSDP I) ambapo, Halmashauri ya kilwa imetekeleza jumla ya miradi 7 ambayo imekamilika na inahudumia vijiji 12, Halmashauri ya Lindi imetekeleza/inatekeleza miradi 7 inayohudumia vijiji 13 kati ya hiyo, miradi 6 imekamilika na mradi 1 unaendelea na ujenzi upo katika hatua za mwisho za majaribio.
Manispaa imetekeleza miradi 7 inayohudumia mitaa 20 na yote imekamilika na kutoa huduma, Liwale imetekeleza jumla ya miradi 6 inayohudumia vijiji 9 ambayo yote imekamilika na kutoa huduma, Nachingwea imetekeleza miradi 7 inayohudumia vijiji 7 na Halmashauri ya Ruangwa imetekeleza miradi 5 ambayo imekamilika na inahudumia vijiji 12. Jumla ya miradi 38 ujenzi wake umekamilika, mradi 1 ujenzi wake upo katika hatua za majaribio, Jumla ya vijiji 71 vinanufaika na huduma ya Maji.
1.1.3 Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji awamu ya II (WSDP II)
Mkoa wa Lindi unatekeleza programu ndogo ya maji na usafi wa mazingira awamu ya II ambapo hadi kufikia Agosti, 2018 hali ya utekelezaji ni kama ifuatavyo:-
1.2 Usajili wa Vyombo vya Watumiaji Maji
Katika kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu, miradi yote inaendeshwa na wananchi wenyewe kupitia Vyombo huru vya Watumiaji Maji/Vikundi vinavyoundwa kisheria (COWSOs). Hadi Juni 2018 julma ya vyombo vya watumiaji Maji 150 vimeanzishwa na kusajiliwa katika Mkoa. Kilwa (22), Lindi (47), Manispaa (2), Liwale (36), Nachingwea (21) na Ruangwa (22).
1.3 Hali ya huduma ya maji mji wa Lindi
1.3.1 Mji wa Lindi
Idadi ya watu wanaopata huduma ya Maji safi ni watu wasiopungua 68,976 sawa na asilimia 75% ya wakazi wote waishio eneo la Manispaa ya Lindi. Hali ya huduma imeimarika, hii ni kufuatia kuanza kutoa huduma kwa mradi mpya wa maji kutoka chanzo cha ng’apa.
Huduma ya maji hutolewa kupitia vyanzo vya maji vya Ng’apa, Mnazi mmoja, Mtange, Tulieni, Mmongo, Sinde na Mbanja, hata hivyo wakazi wengi hulazimika kufuata maji umbali mrefu kupitia Virula(Vioski) kutokana na baadhi ya maeneo kutofikiwa na mtandao wa maji.
1.3.2 Mpango wa Uboreshaji wa Huduma ya Maji katika Mji wa Lindi (Mradi wa Maji Ng’apa)
Serikali imepata ufadhili kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia Millenium Development Goal Initiative wa Euro Milioni 13.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Lindi. Gharama hizi ni pamoja na kazi za nyiongeza (Variations). Mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya Ujerumani kupitia KfW (Benki ya Maendeleo ya Ujerumani)
1.3.2.1 Kazi zilizopangwa kufanyika
Kazi zinazopangwa kufanyika ni: uchimbaji wa visima virefu 10; ujenzi wa chujio (aerator, contact basin/balancing tank, rapid sand filtration, clear water reservoir, high lift pumping station, backwash pumping station) lenye uwezo wa kusafisha maji mita za ujazo 7,500 kwa siku; ujenzi wa matanki mawili ya maji yenye ukubwa wa mita za ujazo 3,000 na 2000, ulazaji wa bomba kuu la maji umbali wa kilomita 11.5 na mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 27; ujenzi wa vituo vya kuchota maji na ujenzi wa mabwawa ya kutibu maji taka na ununuzi wa gari la huduma ya uondoaji majitaka.
1.3.2.2 Hatua iliyofikiwa
1.3.2.3 Kazi zinazoendelea
Kuunganisha mfumo wa automation katika mfumo wa kutibu maji (Water treatment plant)
Kuunganisha mabomba ya usambazaji katika mitaa ya muhimbili, Nachingwea na Rahaleo.
Maeneo ambayo yameanza kupata huduma kutoka mradi wa Maji Ng’apa
Baadhi ya maeneo yanayonufaika ni Mjini kati, Mtanda, Wailes, Mtuleni, Mpilipili kusini, Angola, Majanimapana, Usalama, gerezani, sabasaba, Rada, baadhi ya maeneo ya Mlandege, Nachingwea na Kilimahewa (ambapo kuna vituo vya kuchotea maji).
1.5.3 Mradi wa Maji Ng’apa Mtaa wa Ng’apa na Mtaa wa Mitwero
Katika kuhakikisha huduma ya maji inaboreshwa katika Manispaa ya Lindi, Serikali katika bajeti yake ya 2018/19 imeitengea LUWASA kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi miwili ya maji.
Kwa mradi wa Mtaa wa Ng’apa ambao mchakato wake wa manunuzi unasimamiwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, zoezi la kumpata mkandarasi wa ujenzi lipo katika hatua za mwisho kukamilika.
Lakini pia kwa upande wa mradi wa Mitwero Mamlaka tayari ilishawaisilisha andiko la mradi (Project proposal) Wizarani na kinachosubiriwa ni kupata kibali cha kuendelea na taratibu za manunuzi ili taratibu za kumpata mkandarasi zianze.
Hitimisho
Mradi huu utakapokamilika utazalisha maji mita za ujazo 7500 kwa siku (Lita 7, 500,000 kwa siku) na utaongeza huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika mji wa Lindi.
Hali ya huduma za Maji katika Miji Mikuu ya wilaya
Wastani wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa maeneo ya mjini ni 67.96% na upotevu wa maji ni 32.2 %. Takwimu za kila wilaya zinaonyesha kuwa upatikanaji wa huduma Kilwa Masoko ni 80% na kiwango cha upotevu ni 33%. Manispaa ya Lindi upatikanaji ni 75% na upotevu ni 32%, Liwale upatikanaji ni 58% na upotevu ni 32%, Nachingwea upatikanaji ni 71.4% na upotevu ni 29%, Ruangwa upatikanaji ni 55.4 % na upotevu ni 35%. Upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa unasababishwa na uchakavu wa miundombinu ya maji, wateja kutofungiwa dira za maji na mivujo ya mara kwa mara.
Mikakati ya kupunguza upotevu wa maji
Mkoa wa Lindi unakabiliana na changamoto zifuatazo katika utoaji wa huduma za maji;-
1.6.1 Changamoto za Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini
Upatikanaji wa shida wa vyanzo vya maji. Sehemu kubwa hupatikana maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu au mbali na maeneo ya wakazi hivyo kufanya gharama za ujenzi wa miradi ya Maji kuwa kubwa.
Dhana ya maji kuwa huduma ya bure bado imo miongoni mwa watumiaji maji wa vijijini na hivyo kukwamisha uanzishaji wa vyombo huru vya watumiaji maji.
Upungufu wa watumishi wa maji katika halmashauri na mkoa. Halmashauri zilizo athirika zaidi ni Kilwa, Ruangwa, Lindi DC na Lindi MC
Upatikanaji usiokuwa wa uhakika wa vipuri na vifaa vingine vya miradi ya maji vijijini.
1.6.2 Mipango/Mikakati ya kukabiliana na changamoto
Elimu juu ya Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002 inaendelea kutolewa kwa watumiaji maji vijijini na kuwashirikisha kikamilifu wananchi wanufaika katika hatua za kubuni na kujenga miradi yao ya maji.
Kuhusu upungufu wa watumishi, serikali imeanza kuajiri wahandisi na mafundi mchundo na kuwapeleka katika Mkoa na Halmashauri zetu.
Kuhusu upatikanaji wa vipuri vya mitambo ya maji, Halmashauri zimeshauriwa kuwashirikisha wafanyabiashara waliopo katika maeneo yao ili kuwa tayari kuweka katika maduka yao vipuri vya mitambo ya maji, mabomba ya maji pamoja na viungio vyake.
Halmashauri zinaendelea kuwahimiza wananchi kuvuna maji ya Mvua na zimeanza kutunga sheria ndogo za uvunaji maji ya mvua ili kupunguza tatizo la uhaba wa maji.
Kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji elimu inaendelea kutolewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na kuwaondoa wale wote wanaolima karibu na vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuwachukila hatua za kisheria wanaochoma moto maeneo yenye vyanzo vya maji ikiwemo ufyatuaji wa matofali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.