SEKTA YA ELIMU
Mkoa wa Lindi wenye halmashauri 6 unazo taasisi mbalimbali za elimu zilizoanzishwa na serikali kwa lengo la kujenga taifa la watu thabiti, wenye misingi bora ya malezi, maadili, ujuzi, umahiri na uwezo wa kujitegemea katika dunia ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia (Sera ya Elimu na Mafunzo 2014).
Taasisi zenye dhamana ya utoaji elimu zilizopo katika Mkoa wa Lindi ni shule za msingi 498, shule za sekondari 122, chuo cha ualimu 1, vyuo vya maendeleo ya jamii 2, chuo cha VETA 1, chuo kikuu huria 1, taasisi ya elimu ya watu wazima 1, vituo vya ufundi stadi 14 na shule zenye mkondo maalum 6 na vituo vya MEMKWA 49. Pamoja na taasisi zilizotajwa kuna shule shikizi (satellite schools) 44 ambapo kila halmashauri ina shule za namna hiyo ambazo baadaye zitakuwa shule kamili.
TAARIFA ZA WANAFUNZI
Mkoa una jumla ya wanafunzi wa shule za msingi (darasa la I – VII) 202,762 wakiwemo wavulana 100,807 na wasichana 101,955. Kwa upande wa elimu ya sekondari wanafunzi waliopo ni 29,222 wakiwemo wavulana 14,864 na wasichana 14,358. Wanafunzi waliopangwa kujiunga kidato cha tano walikuwa 1,462 na walioripoti mpaka tarehe 18 Septemba, 2017 ni 1002. Hivyo, wanafunzi 460 hawakuripoti kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubadilishiwa shule na wengine kujiunga na shule za binafsi.
Taarifa ya uandikishaji kwa mwaka 2017, kwa wanafunzi wa awali maoteo yalikuwa 29,920 (wav 14,828 na was 15,092), uandikishaji halisi ni 29,567 sawa na asilimia 99 (wav 14,524 na was 15,043). Wanafunzi wa darasa la kwanza maoteo 28,667 (wav 14,495 na was 14,172) uandikishaji halisi ni wanafunzi 36,246 sawa na asilimia 126.4 (wav 18,527 na was 17,719.
TAARIFA ZA WALIMU
Ili ufundishaji na ujifunzaji uwe fanisi na wenye matokeo chanya kunahitajika pawepo na walimu wenye umahiri kwa ajili ya kutoa maarifa kwa wanafunzi waliopo. Mahitaji ya walimu kwa elimu ya msingi ni 5,104, walimu waliopo ni 3,721 na upungufu ni 1,383. Katika elimu ya sekondari upungufu wa walimu upo kwa walimu wa sayansi ambapo mahitaji halisi ni walimu 716, waliopo 243 na upungufu ni walimu 473 ambao ni sawa na 66.1%.
Katika jitihada za serikali za kuajiri walimu wapya, mkoa ulipangiwa walimu 103 wa sayansi awamu ya kwanza mwezi Aprili, 2017 na walioripoti ni walimu 96, walimu 7 hawakuripoti. Awamu ya pili mkoa ulipangiwa walimu 17 wa sayansi na hisabati na walioripoti ni walimu 8 na wasioripoti ni walimu 9. Mkoa hauna upungufu wa walimu wa masomo ya sanaa.
MIUNDOMBINU YA SHULE ILIYOPO
Miundombinu ni eneo muhimu sana katika kufanikisha suala zima la ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi. Katika elimu ya msingi mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 4,908 na vilivyopo ni 3,101 na upungufu ni 1,804. Kwa upande wa nyumba za walimu mahitaji ni nyumba 4,262 zilizopo 1,270 na upungufu 2,993.
Kwa upande wa elimu ya sekondari kuna upungufu wa miundombinu kama ifuatavyo: mahitaji ya vyumba vya madarasa 833, vilivyopo 800 na upungufu 33, nyumba za walimu mahitaji ni 1,628, zilizopo 390, upungufu 1,238, vyumba vya maabara mahitaji ni 345 vilivyopo 114 na upungufu 231. Aidha, katika matundu ya vyoo pia kumekuwa na upungufu mkubwa ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopo kwa elimu ya msingi na sekondari.
MIRADI INAYOYOTEKELEZWA KATIKA MKOA
Mkoa umekuwa ukitekeleza miradi/programu mbalimbali ikiwemo EQUIP- Tanzania katika halmashauri zote 6. Mpaka mwezi Agosti, 2017 kiasi cha Tsh. 8,458,143,629 kilipokelewa katika halmashauri za mkoa huu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za program ya Equip-T. Programu ya LANES inatekelezwa katika halmashauri ya Wilaya ya Liwale (shule shikizi 10) na ikihusika na vituo vya MEMKWA kwa halmashauri 6. Pia miradi chini ya mpango wa EP4R inayohusika na fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mkoa umekuwa ukisimamia kwa karibu kuhakikisha dhima ya serikali inafikiwa.
UENDESHAJI WA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2017
Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2017 umefanyika kuanzia tarehe 6 na 7 Septemba, 2017 nchini kote. Kwa mkoa wa Lindi mtihani huu umefanyika katika shule 480 zenye jumla ya wanafunzi 17,519 wakiwemo wavulana 8,117 na wasichana 9,402 katika halmashauri 6 za mkoa wa Lindi. Aidha, mtihani huo ulifanyika katika mazingira ya utulivu, amani na usalama katika halmashauri zote.
TAARIFA ZA WATAHINIWA
Waliosajiliwa na waliofanya Mtihani
Jumla ya Wanafunzi 26,804 waliandikishwa kuanza darasa la I mwaka 2011, wanafunzi 17,519 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2017. Aidha, wanafunzi 17,392 (99.3%) walifanya Mtihani na wanafunzi 127 (0.7%) hawakufanya Mtihani huo kutokana na sababu mbalimbalikama inavyooneshwa katika jedwali na 1 na 2.
JEDWALI NA 1: MCHANGANUO WA WANAFUNZI WALIOFANYA MTIHANI
Halmashauri
|
WALIOANDIKISHWA 2011
|
WALIOSAJILIWA
|
WALIOFANYA MTIHANI
|
|||||||
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
%
|
|
Kilwa
|
3080
|
3050
|
6130
|
1931
|
2107
|
4038
|
1901
|
2078
|
3979
|
98.5
|
Lindi
|
2974
|
3303
|
6277
|
1629
|
2010
|
3639
|
1614
|
1993
|
3607
|
99.1
|
Lindi Manispaa
|
1006
|
1036
|
2042
|
729
|
815
|
1544
|
729
|
813
|
1542
|
99.9
|
Liwale
|
1452
|
1497
|
2949
|
1031
|
1169
|
2200
|
1026
|
1167
|
2195
|
99.6
|
Nachingwea
|
2617
|
2673
|
5290
|
1705
|
1894
|
3599
|
1696
|
1883
|
3579
|
99.4
|
Ruangwa
|
2085
|
2031
|
4116
|
1092
|
1407
|
2499
|
1086
|
1404
|
2490
|
99.6
|
JUMLA
|
13214
|
13590
|
26804
|
8117
|
9402
|
17519
|
8052
|
9338
|
17392
|
99.3
|
JEDWALI NA 2: MCHANGANUO WA WANAFUNZI WASIOFANYA MTIHANI
Halmashauri
|
UTORO
|
VIFO
|
UGONJWA
|
SABABU NYINGINE
|
JUMLA
|
||||||||||
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
|
Kilwa
|
27
|
19
|
46
|
1
|
1
|
2
|
2
|
2
|
4
|
0
|
7
|
7
|
30
|
29
|
59
|
Lindi
|
15
|
10
|
25
|
0
|
0
|
0
|
0
|
1
|
1
|
0
|
6
|
6
|
15
|
17
|
32
|
Lindi Manispaa
|
0
|
1
|
1
|
0
|
0
|
0
|
0
|
1
|
1
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
Liwale
|
4
|
2
|
6
|
1
|
0
|
1
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
5
|
2
|
7
|
Nachingwea
|
8
|
8
|
16
|
1
|
0
|
1
|
0
|
3
|
3
|
0
|
0
|
0
|
9
|
11
|
20
|
Ruangwa
|
3
|
3
|
6
|
3
|
0
|
3
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
0
|
6
|
3
|
9
|
JUMLA
|
57
|
43
|
100
|
6
|
1
|
7
|
2
|
7
|
9
|
0
|
13
|
13
|
65
|
62
|
127
|
Aidha, kwa mwaka 2017, Mkoa wa Lindi una jumla ya Wanafunzi 35 wakiwemo wavulana 17 na wasichana 18 ambao hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu waliofanya mtihani huu.
MAANDALIZI YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) MWAKA 2017
Mkoa umeendelea na maandalizi ya kufanyika kwa mtihani huo kwa kuendelea kusimamia ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya shule kwa kila mwalimu. Walimu wakuu, waratibu elimu kata, wakaguzi na maafisa elimu ngazi ya wilaya wamekuwa wakisisitizwa kusimamia na kuhakikisha kazi ya ufundishaji na ujifunzaji inafanyika kikamilifu. Pia mkoa umeendesha mtihani wa dhihaki kwa shule zote za sekondari za serikali na zisizo za serikali na kutoa matokeo. Katika mtihani huo watahiniwa 3,878 kati ya watahiniwa waliosajiliwa 4,010 walifanya matihani.
Matokeo ya mtihani huo yanaonesha ufaulu wa daraja I – III ni watahiniwa 636 (16.4%), daraja la IV ni watahiniwa 2187 (56.4%) na daraja la 0 wamepata watahiniwa 1050 (27.1%). Halmashauri pia zimekuwa na mitihani inayoendeshwa na kusimamiwa vyema ikiwa ni jitihada za kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne utakaofanyika mwezi Novemba mwaka 2017 nchini kote. Jitihada zinazofanyika kwa kidato cha nne pia zimekuwa zikisisitizwa kufanyika kwa vidato vyote ngazi ya shule.
MAANDALIZI YA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018
Mkoa wa Lindi wenye jumla ya shule za sekondari 116 zilizo za serikali unatarajia kupokea wanafunzi 17,392 (99.3%) wa kidato cha kwanza mwaka 2018. Idadi hiyo ya wanafunzi ndio waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2017. Hivyo basi, vyumba vya madarasa vitakavyohitajika kwa ajili ya wanafunzi hao ni 435 ikilinganishwa na vyumba 246 vilivyohitajika mwaka 2017 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wapatao 9,879 (65.16%) waliofaulu. Ili kuepukana na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ni wajibu wa kila halmashauri kufanya maandalizi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mapema kabla ya zoezi la uchaguzi wa wanafunzi hao halijafanyika.
Mwezi Januari, 2017 halmashauri ya Kilwa (shule ya sekondari Kilwa Kivinje, Ali Mchumo, Kiranjeranje na Mpunyule) na halmashauri ya Ruangwa (shule ya sekondari Ruangwa, Chinongwe, Mnacho, Namichinga na Hawa Mchopa) zilikuwa na miundombinu pungufu iliyopelekea wanafunzi waliofaulu kubaki bila kupangwa. Hivyo, ni jukumu la kila halmashauri kujiandaa kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi hao ili isije ikajitokeza wakati wa zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 wanafaunzi wanabaki bila kupangwa katika shule husika kwa kukosa vyumba vya madarasa.
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA ELIMU
Mkoa wa Lindi katika utekelezaji wa kazi za Sekta ya elimu unakumbana na changamoto mbalimbali miongoni mwa changamoto hizi ni: -
MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO KATIKA SEKTA YA ELIMU NA KUINUA TAALUMA KATIKA MKOA
Baadhi ya mikakati ya kukabili changamoto za sekta ya elimu katika mkoa ni pamoja na;
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.