Katika jitihada za kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka na utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi unazingatiwa , Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na Halmashauri zake umeazimia kutoa na kuinua elimu kwa wanafunzi wote . Ili kufanikisha azma hii, Mkoa umeandaa Mpango Mkakati wa Elimu kwa mwaka 2025 ambapo umebainika mfumo wa Shirikishi wa ufuatiliaji katika sekta ya Elimu wenye kuanisha changamoto 14.
Hivyo, Leo Mei 2, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amezindua Mpango Mkakati wa Elimu 2025 huku akisisitiza walimu na wasimamizi wa sekta za Elimu kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Elimu wa mwaka 2025 ili kuendelea kuboresha Elimu na ufaulu wa Mkoa katika Mitiani na pimaji za Kitaifa kwa mwaka 2025.
Mpango wa Mkakati wa Elimu 2025 unakwenda kuongeza hamasa na chachu kwa wadau wa elimu kwa kuimarisha mifumo mbalimbali ya utendaji wa kazi kama vile utoaji wa taarifa na takwimu, Uteuzi wa walimu viongozi walio madhubuti na ufuatiliaji shirikishi wa ufundishaji , usimamizi wa utekelezaji wa mfumo wa utendaji wa kazi , utoaji wa huduma bora kwa walimu na wanafunzi, kuwa na malengo ya ufundishaji unaojenga maana, kuongea na kuwa karibu na wanafunzi , walimu na wazazi, kuwaelimisha wadau wa elimu kuyatambua majukumu yao na kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuleta ufanisi katika mkoa wa Lindi na kuratibu na kusimamia ubora wa upimaji wa mitihani iliyoandaliwa kuanzia ngazi ya shule , kata , wilaya na Mkoa.
kwa kuzingatia maelekezo ya Miongozo mitatu ya elimu iliyozinduliwa Agosti, 2022, Mikataba ya utendaji kazi na maelekeo ya Mpango Mkakati wa Elimu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya kufanya tathmini na ufuatiliaji wa namna ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Akizungumza kabla ya kuzindua na kuwakabidhi mpango Mkakati wa Elimu Mkoa wa Lindi 2025 waheshimiwa wakuu wa Wilaya, Mhe. Telack amesisitiza ushirikiano katika kufanikisha mpango huo.
"Nitoe wito kwa wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia kwa ufanisi utekelezaji wa mpango huu kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Elimu, Walimu, Wazazi pamoja na wadau wengine " Mhe. Zainab Telack
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.