• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Madini

SHUGHULI ZA MADINI KWA MKOA WA LINDI

 

UTANGULIZI

Sekta ya madini ni sekta inayoanza kukua kwa kasi katika mkoa wetu pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili kama ukosefu wa miundombinu ya barabara, maji, huduma za jamii na umeme wa uhakika katika maeneo madini yanapopatika. Kukua huku kumetokana na usimamizi mzuri wa mkoa kwa kushirikiana na kamishna wa madini, wananchi, wadau na uwepo wa madini ya aina mbalimbali, kukua kwa teknolojia na uwepo wa wawekezaji wakubwa na wadogo katika sekta hii.

AINA ZA LESENI

Aina A: LESENI ZA UTAFITI (PLs)

  • Leseni ya utafiti (Prospecting Licence): Ina uhai wa miaka 4, ikihuishwa mara ya kwanza miaka 3, ikihuishwa mara ya pili miaka 2. Leseni hii hutolewa na Kamishna wa Madini, DSM. Kiwango cha juu cha ukubwa wa leseni hizi na kilometa za mraba 300 (50% relinquishment)
  • Leseni ya utafiti ya Vito isipokuwa almasi: Ina uhai wa mwaka mmoja na haihuishwi. Leseni hii hutolewa na Kamishna wa Madini, DSM. Ukubwa usiozidi kilometa za mraba 5
  • Leseni ya Utafiti wa madini ya ujenzi: Ina uhai wa mwaka mmoja na haihuishwi. Leseni hii hutolewa na Kamishna wa Madini, DSM. Ukubwa usiozidi kilometa za mraba 5
  • Leseni ya kuhodhi eneo (Retention Licence): Leseni ni ya miaka mitano na inaweza kuhuishwa kwa miaka mingine mitano. Leseni hii hutolewa na Waziri wa Nishati na Madini endapo hali ya uchumi hairuhusu kuanza uchimbaji katika eneo lililofanyiwa utafiti

AINA B: LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI 

  • Leseni ya uchimbaji wa kati (ML): Hutolewa kwa miaka 10 na inahuishwa kwa miaka mingine 10. Hutolewa na Waziri wa Nishati na Madini. Ukubwa usiozidi kilometa za mraba 10.
  • Leseni Kubwa ya uchimbaji Madini (SML): Hutolewa kwa miaka 25 na inahuishwa kwa miaka mingine 25. Hutolewa na Waziri wa Nishati na Madini. Ukubwa usiozidi kilometa za 35 kwa madini ya kwenye miamba na usiozidi kilometa za mraba 70 kwa madini ya tabaka lilitokana na kusagika kwa miamba (superficial deposit)

AINA C: UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI (PMLs)

Leseni za uchimbaji mdogo wa madini (PMLs): Zina uhai wa miaka 7 kwa madini yenye uchimbaji wa muda mrefu (zina ukubwa wa hekta 10) na mwaka mmoja kwa leseni leseni zenye uhai mfupi mfano mchanga na kifusi (zina ukubwa wa hekta 5 kiwango cha juu). Hizi ni kwa Watanzania tu. Zinahuishwa kwa miaka mingine saba na huombwa upya kwa zile za mwaka mmoja. Leseni hizi hutolewa na Afisa Madini Kanda. 

AINA D: UCHENJUAJI WA MADINI

  • Leseni za kuchenjua madini (Processing Licence): Hutolewa na Kamishna wa Madini na zina uhai wa miaka 10 na zinahuishwa kwa kipindi kingine cha miaka 10
  • Leseni za kuyeyusha/Kuchoma madini (Smelting Licence): Hutolewa na Waziri na zina uhai wa miaka 25 na zinahuishwa
  • Leseni za kusafisha madini (Refining Licence): Hutolewa na Waziri na zina uhai wa miaka 25, pia zinahuishwa

LESENI ZA BIASHARA YA MADINI

  • Leseni Kubwa ya Biashara ya Madini (Dealers licence): Hutolewa na Afisa Madini Kanda na huisha tarehe 30/06 ya kila mwaka na huombwa upya.
  • Leseni ndogo ya biashara ya Madini (Broker’s licence): Hutolewa na Afisa Madini Kanda na huisha tarehe 30/06 ya kila mwaka na huombwa upya. Hii ni kwa Watanzania tu na haimruhusu mmiliki kuuza madini nje ya nchi.

MADINI YAPATIKANAYO MKOA WA LINDI

  • Lindi: Madini ya ujenzi, chumvi, mawe ya chokaa, feldspar, pozzolana, Makaa ya mawe, chuma, jasi, kinywe (graphite),
  • Kilwa: Jasi, mawe ya chokaa, madini ya ujenzi, chuma, vito, kinywe
  • Ruangwa:  Dhahabu, vito, kinywe, madini ya ujenzi, chuma, shaba, feldspar, Garnet (RED & GREEN).
  • Liwale: Dhahabu, nikeli, mabo (marble), manganese, amazonite.
  • Nachingwea: Dhahabu, kinywe, vito, chuma, shaba, Nikeli

  

AINA NA IDADI YA LESENI ZILIZO HAI MPAKA SASA

Eneo/Mahali
PMLs
PLs
MLs
SMLs
RLs
Jumla
Lindi Vijijini
189
Chumvi, Madini ya Ujenzi, Jasi na madini mengine
6
Chokaa, Jasi, Kinywe na Madini mengine
-
-
-
195
Lindi Mjini
99
Chumvi, Madini ya Ujenzi, Chokaa
2
Chokaa
-
-
-
101
Kilwa
1231
Chumvi, Madini ya Ujenzi,  Jasi, Chokaa, Madini Mengine
22
Dhahabu, Mchanga, Chokaa, Kinywe, Jasi na Madini mengine
7
Jasi
-
-
1260
Ruangwa
278
Vito, Dhahabu, Kinywe, Shaba, Chuma, Madini ya Ujenzi na Madini mengine
28
Dhahabu, Shaba, Kinywe, Nikeli
9
Dhahabu, Kinywe na Vito
1
Kinywe
-
316
Nachingwea
156
Vito, Dhahabu, Kinywe, Shaba, Chuma, Madini ya Ujenzi na Madini mengine
14
Dhahabu, Shaba, Kinywe, Nikeli na Chuma
1
Vito
-
1
Nikeli
172
Liwale
162
Vito, Dhahabu na Madini mengine
30
Dhahabu, Manganese,  Uranium na Nikeli
2
Dhahabu
-
-
194
Zinazoingiliana Mpika ya Wilaya za Lindi na baadhi Mtwara
-
44
Jasi, Dhahabu, Nikeli, Shaba, Kinywe, Chokaa, Makaa ya Mawe na Madini mengine
-
-
-
44
Jumla1
2115
146
19
1
1
2282


www.mem.go.tz

www.portal.go.tz

www.portal.go.tz/map

Sophiaa S. Omary - 0764054316

Ogesa C. Tale – 0755 528 528

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.