Upo uhamisho wa aina mbili kwa maana ya uhamisho wa wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari
Kwa Shule za Msingi unatakiwa
1. Hatua ya kwanza ni kuanzia ngazi ya shule anayosoma ambapo atajaziwa fomu
2. Upitie kwa Mratibu Elimu Kata wa shule anayotoka apitishe fomu
3. Fomu ya Uhamisho ipitishwe na Afisa Elimu Wilaya
4. Fomu iletwe Mkoani kwa ajili ya kupitishwa na Afisa Elimu Mkoa.
Kwa Shule za Sekondari unatakiwa
1. Andika barua ya kuomba nafasi kwenye Shule unayotaka mwanafunzi ahamie. Kama nafasi ipo barua ikipitishwa;
2. Ipeleke barua kwenye shule anayotoka mwanafunzi ili ipitishwe na Mkuu wa Shule na ikishapitishwa
3. Ipeleke kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri anakotoka mwanafunzi ili naye aipitishe
4. Leta maombi yako hayo kwa Katibu Tawala Mkoa kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.