Mkuu wa Wilaya ya Lindi- Victoria amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack na kuanza kuukimbiza 26/05/2025 Halmashauri ya Mtama ambayo itafuatiwa na Manispaa ya Lindi 27/05/2025 Katika Halmashauri ya Mtama Mwenge wa Uhuru umekimbizwa jumla ya Kilomita 153 na kutembelea jumla ya Miradi 7, sambamba na kuweka Mawe ya Msingi, Kuzindulia na kukagua miradi ya maendeleo- Kazi kubwa na nzuri ya kuonekana ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan iliomulikwa na Mwenge wa Uhuru kuangaza miradi ya maendeleo yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 2.7 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Comrade Ismail Ussi sambamba na vijana wazalendo wakimbiza mwenge wameanza kazi Njema ya kuangaza miradi ya Afya, Elimu, Maji, Miundombinu, Miradi ya Vijana, Miradi ya Mapato ya Ndani. Sambamba na hapo- Kongamano kubwa la Vijana lililofanyika katika Kata ya Nyangao ambalo Mtoa Mada Mkuu akiwa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda. Kauli Mbiu: “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.