Balozi wa Japani nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa jana tarehe 15 Juni 2023 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack na kufanya nae mazungumzo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji za Mkoa wa Lindi.
Mhe. Telack amemkaribisha Balozi Misawa ofisini kwake Mkoani Lindi mapema Leo baada ya Kiongozi huo wa kimataifa kuwasili Mkoani Lindi kwa ziara ya Siku moja.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Telack amemueleza Balozi. Msawa fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Lindi ikiwemo uzalishaji mkubwa wa ufuta bora unaojulikana kama Lindi White. Amesema kuwa Kati ya ufuta wote unaozalishwa Tanzania, Mkoa wa Lindi unaozalisha takribani theluthi mbili ya ufuta wote.
Mhe. Telack amemueleza Balozi. Misawa kuwa sekta ya Kilimo ina fursa kubwa ya Uwekezaji hasa kwenye kuchakata mazao ya biashara yanayolimwa Mkoani Lindi ikiwemo ufuta pamoja na korosho.
Pamoja na fursa za kilimo, Mhe. Telack amemueleza mgeni wake juu ya uwepo wa fursa za madini, uvuvi, kilimo cha mwani na utalii.
Kwa upande wake, Balozi. Misawa amesema kuwa amefurahishwa na ubora wa ufuta unaozalishwa Mkoani Lindi kwani amezisikia sifa zake nzuri.
Aidha, Balozi . Misawa amevutiwa kwa kiasi kikubwa na fursa za uvuvi hasa katika Wilaya ya Kilwa ambapo amesema kuwa kama uwekezaji utafanyika katika kuboresha Teknolojia za uvuvi na miundombinu ya kuhifadhia samaki, sekta ya uvuvi itakuwa na matokeo makubwa
Balozi. Misawa amehitimisha ziara yake Mkoani Lindi ambapo pamoja na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa pia ametembelea ghala kuu la Moledina lililopo Lindi Mjini qna kujionea shughuli ya ukusanyaji wa ufuta kutoka vyama vya Msingi vya Lindi Mwambao. Pia amepata nafasi ya kukitembelea Chuo cha Ufundi Stadi, VETA na kujionea programu za mafunzo zinazotolewa na chuo hicho.
ReplyForward |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.