Jana Jumanne Balozi wa nchi ya Uturuki hapa Tanzania Mhe. Mehment Gu”lluoglu ametembelea Mkoani Lindi akiambatana na wafanyabiashara kutoka Uturuki. Mhe. Balozi amefanya ziara ya siku moja Mkoani Lindi maalum kwa ajili ya kufungua fursa mbalimbali zilizopo hapa Tanzania, Mkoani Lindi na nchi ya Uturuki.
Katika kikao kifupi kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kilichowajumuisha viongozi wa mkoa, wilaya, kamati ya usalama mkoa na wafanyabiara kutoka nchini Uturuki Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Telack na Balozi. Mhe. Mehment wote wawili waliwasilisha fursa zilizopo kwenye maeneo yao.
Mhe. Telack akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao kumalizika ameeleza kuwa mkoa umetangaza fursa zilizopo ndani ya mkoa ikiwemo madini, mazao ya biashara ya ufuta na korosho, uvuvi, fukwe nzuri na fursa kubwa ya gesi asilia.
“Tumewaeleza kile ambaccho tunacho ndani ya mkoa wa Lindi…tuna madini, madini yote ukiacha almasi , dhahabu ambayo purity yake 98%, graphite ambayo ipo mkoa mzima, manganese, Uranium, Cobalt……. na vito vyote ambavyo mnavifaham vipo.” Amesema Mkuu wa Mkoa.
Akionyesha kufurahishwa na fursa zilizopo mkoani Lindi hasa zao la korosho na ufuta pamoja na mazingira ya Lindi kwa ujumla, Balozi. Mhe. Mehment amesema ziara hii imekuwa na tija katika kuiunganisha nchi ya Tanzania na Uturuki kupitia Nyanja ya biashara na uwekezaji.
Katika ziara yake Mhe. Balozi mkoani Lindi ametembelea na kijionea shughuli mbalimbali za kiuchumi kwenye ghala kuu la korosho BUKO, Mchinga, soko la samaki pwani ya NBC, Chuo cha Ufundistadi (VETA) pamoja na eneo la mradi wa gesi asilia, Likong’o.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.