Balozi wa Zimbabwe hapa nchini Tanzania Mhe. Lt. Jen. Anselim Nhamo Sanyatwe leo jumanne amefika Mkoani Lindi na kukutana na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi ofisini kwake.
Balozi Sanywate amemueleza Katibu Tawala Ndg. Ngusa Samike kuwa amefika Mkoani Lindi kwa ziara Maalum ya kutembelea kambi za mafunzo zilizosaidia katika Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Zimbabwe.
Balozi Sanywate ameongeza kuwa pamoja na kutembelea kambi hizo lakini pia ziara ina lengo la kutafuta fursa za Uwekezaji Kati Nchi ya Zimbabwe na Tanzania.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa Ndg. Ngusa Samike amemshukuru Balozi Sanywate kwa kufika Mkoani Lindi, hii ni kuonesha kuwa Tanzania na Zimbabwe ni ndugu wa karibu.
Balozi Sanywate ameanza ziara yake Mkoani Lindi ambapo atafanya kazi kwa siku mbili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.