• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

BIL 7.8 KUKAMILISHA UJENZI WA MIRADI YA ELIMU MTAMA DC , RAS LINDI ASISITIZA KUKAMILIKA KWA WAKATI

Posted on: January 8th, 2025

Shilingi bilioni 7.8 zinatarajiwa kutumika kujenga na kukarabati miradi mbalimbali ya sekta ya elimu katika Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 4.1 zinatoka serikali kuu, bilioni 3 kutoka kwenye Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), na milioni 719 kutoka kwenye Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya wavulana kanda ya Kiwalala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mahumbika, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Chiuta, na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mandwanga. Pia kutakuwa na ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mtakuja, ukarabati wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Navanga, na ujenzi wa Shule ya Amali Mpenda.
Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa matano katika Shule ya Msingi Simana, ujenzi wa Shule ya Sekondari Mtakuja katika Kata ya Nyangao, ujenzi wa shule mpya ya amali mkoa, na ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata ya Pangani.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua uendelevu wa miradi hiyo na kuona maandalizi ya kuripoti kwa wanafunzi wa darasa la kwanza, awali, na kidato cha kwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Zuwena Omary, ametoa wito kwa menejimenti ya halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Aidha, amesisitiza kuhakikisha wanafunzi wote waliopangiwa na kuandikishwa wanaripoti shuleni kwa wakati..

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama  Anderson  Msumba amesema wanamshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi alizowaletea , kwa mara ya kwanza kupata fedha nyingi kama hizo na amwakikishia Katibu Tawala Mkoa kukamilisha miradi hiyo mwishoni mwa mwezi wa Nne.

Mwakilishi wa wenyeviti kutoka Halmashauri ya Mtama Juma Omari Salumu wa kijiji cha Kiwalala amemshukuru Mhe. Rais kwa mradi huo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi na viongozi wote.

Brigita John Mponda mkazi wa kijiji hicho kwaniaba ya wananchi amesema miradi hiyo wameipokea vizuri miradi  ujenzi wa shule mpya kwani inakwenda kuwaletea elimu bora kwa watoto wao.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.