Bodaboda watakiwa kufuata sheria
Waendesha pikipiki (bodaboda) watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili waweze kujiepusha na ajali zinazosababishwa na uzembe.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakati alipokuwa katika ziara yake kwenye manispaa ya Lindi ambapo alisisimama kwenye kituo cha bodaboda katika mtaa wa mnazi mmoja na kubaini mapunguvu ya pikipiki wanazotumia.
Baada ya kisimama katika kituo hicho kilichokuwa na pikipiki zaidi ya 15, Zambi alimuamuru ofisa polisi kutoka ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Lindi, Inspekta Mohamedi kufanya ukaguzi wa madereva pamoja na pikipiki zao.
Asilimia kubwa ya madereva walikuwa hawana lesini inayowaruhusu kuendesha chombo chochote cha moto, hawana kofia mbili ngumu (helement) kwa ajili ya dereva na abiria, pikipiki hazina bima, na kutovaa mavazi yanayotakiwa kwa usalama wao.
Mkuu wa Mkoa Zambi alitoa wiki moja kwa wamiliki/madereva bodaboda hao kuhakikisha wanalipia bima pikipiki zao, kukata lesini zitakazowaruhusu kuendesha vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wataratibu nyingine zote zinazokakiwa.
Aidha, alimuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya hiyo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara baada ya muda alioutoa kukamilika. Pia alilitaka jeshi hilo kuwachukulia hatua kali madereva na wamiliki wa vyombo hivyo ambao watakuwa hawajatekeleza agizo hilo.
Pamoja na agizo hilo Mkuu wa Mkoa Zambi amewataka madereva wote wa pikipiki hizo za biashara kuhakikisha wanakata vitambulisho vya ujasiriamali kama agizo la serikali lilivyotolewa. Aliwaeleza kuwa kitambulisho hicho ni muhimu kwao ambapo pia aliwatajia faida za kuwa na kitambulisho hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.