Maelekezo hayo yametolewa jana jumapili na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack katika kikao cha wadau cha tathmini ya msimu wa korosho Kwa mwaka 2022/23 na maandalizi ya msimu wa ufuta 2023/24 kilichofanyika Wilaya ya Nachingwea, ukumbi wa Chuo cha Ualimu.
Mhe. Telack amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa miti ya mikorosho iliyopo mashambani kwa kiasi kikubwa haina tija hivyo ni vyema ikafanyiwa maboresho kwa kuibebesha.
Mhe. Telack ameongeza kuwa ili kufikia malengo ya kuongeza uzalishaji na kipato kwa mkulima, Bodi ya Korosho ni wakati sasa wa kutoka na kwenda kwa wakulima kutoa elimu ya faida ya kubebesha miti ya Korosho ili iweze kuwanufaisha.
Akitoa ushuhuda wa faida ya ubebeshaji wa mikorosho, Mhe. Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Lindi amesema kuwa ubebeshaji wa mikorosho ukifanyika Kwa wakati kuanzia mwezi Novemba mpaka Desemba matokeo yake yanaanza kuonekana mapema mwanzoni mwa mwaka unayofuata.
Mhe. Ndemanga ameendelea kueleza kuwa mmea uliobebeshwa unazaa mapema na Kwa uwingi Sana kiasi ambacho mmea unaweza kushindwa kuhimili uzito wa mazao hayo, hivyo ni lazima mkulima ahakikishe anaufuatilia na kuuwekea vizuizi ili usivunjike.
Pia amewataka Bodi ya Korosho Tanzania, kuwatafuta na kuwatambua Vijana wote wenye elimu ya ubebeshaji wa mikorosho ili waisambaze elimu hiyo kwa wakulima. Mhe. Ndemanga ameongeza kuwa vijana hao wapo maeneo mengi ya kanda ya Kusini lakini hawafahamiki.
Akimuwakilisha Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho kwenye kikao hicho, Ndg.Juma Yusuph Mpili Kaimu Meneja wa Mipango ya Kilimo, amesema kuwa zoezi la ubebeshaji wa mikorosho litaanza punde tu uvunaji wa korosho utakapokamilika kuanzia mwezi Desemba.
Ndg. Mpili ameongeza kuwa sambamba na ubebeshaji wa mikorosho, zoezi la uzalishaji wa miche ya korosho Kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima litaanza msimu ujao wa mwaka 2023/24. Ameongeza kuwa kwa sasa Bodi ya Korosho inaandaa vifaa kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.