Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema kuwa serikali imetekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 kwa kuchangia huduma za afya katika kiwango kikubwa.
Zambi ameyasema hayo katika uzinduzi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliofanyika katika uwanja wa Ilulu – Manispaa ya Lindi ambapo alikuwa mgeni rasmi. Uzinduzi huo licha ya kuhudhuriwa na viongoizi mbalimbali, pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya, Mama Anna Makinda.
Serikali imetekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 kupitia NHIF kwa kuchangia katika kiwango kikumbwa vifaa vya kutoa huduma katika vituo vyakutolea huduma za Afya. Hospitali ya Rufaa ya mkoa Sokoine imenufaika na mfuko huo kwa kupata mkopo wa shilingi milioni 266 na kununua vifaa kwajili ya matumizi ya hospitali.
Pia zambi ametoa tamko la kwamba katika mfuko huu wa Bima ya Afya yeye atakuwa balozi wa kwanza wa kuamasisha wananchi pamoja na makundi mbalimbali kijiunga na kuchangia mfuko huu wa bima ya Afya na Bima ya Afya ya jamii iliyoboreshwa kwani utakuwa msaada kwao juu ya matibabu katika kipindi chote cha maisha. Aidha, Zambi amehaidi kuwa balozi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika mkoa wa Lindi.
Pia mwenyekiti wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya,Mama Anna Makinda amesema wafanyabiashara ni muda wao sasa kujiunga katika mfuko huu wa Taifa wa bima ya Afya kwani utawasaidia katika kipindi chote cha kufanya biashara hata watakapo anguka kibiashara wasipate shida juu ya matibabu na popote watakapo kwenda watapata huduma ya Afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.