Mafisa kutoka Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) wakiongozwa na Mkuu wa Chuo Dkt. Tumain Gurumo wamemweleza Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack juu ya ujio wao Mkoani humo kuhusu kuendesha Mafunzo ya elimu ya usalama kwa wavuvi zaidi ya 10 na mpango Mkakati wa kujenga tawi la Chuo Cha Bahari Dar Es Salaam (DMI) eneo la kikwetu.
Hayo, wameyaeleza walipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ofisini kwake, Agosti 20, 2024 kwa lengo la kujitambulisha na kutambulisha programu yao .
Maafisa wanatarajia kuendesha mafunzo ya kampeni ya utoaji elimu ya usalama kwa wavuvi zaidi ya elfu 10 wanaofanya shughuli zao za uvuaji wa samaki katika Mkoa wa Lindi ili kufikia lengo la kuleta ufahamu juu ya masuala ya usalama wa baharini kwa wavuvi na wananchi kwa ujumla.
Wakieleza mpango wa ujenzi wa chuo hicho, wamewasilisha ombi la kuongezewa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi, ambapo wametakiwa kuiandikia barua Manispaa ya Lindi kwa ajili ya utekelezaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amepongeza kampeni ya kutoa elimu ya usalama kwa wavuvi na mchakato wa ujenzi wa chuo cha bahari, kwani chuo hicho kitakuwa na tija kubwa kwa wananchi wa Lindi na watanzania kwa ujumla .
"tunabahari ambayo bado hatujavuna matunda yake vizuri kama ambavyo tunavuna katika kilimo , chuo hicho naamini kitaleta mabadiliko chanya kwa wananchi " Mh. Telack
Maafisa wa DMI wataendelea na mafunzo kwa muda wa wiki moja ndani ya Mkoa wa Lindi.
UJENZI WA BANDARI YA UVUVI YA KISASA WAFIKIA 72% WILANI KILWA LINDI.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.