Katika kikao cha ukusanyaji wa maoni ya wadau kuhusu Dira ya Taifa 2050, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewakumubusha wadau kuwa Nchi imepata utulivu na kupiga hatua za kimaendeleo kwasababu ya uwepo wa amani, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anadumisha amani ya Tanzania hasa katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu wa mwakani 2025.
" Amani, utulivu nausalama wa rai na mali zao, ni mazingira muhimu kabisa katika maendeleo, bila hayo, dira hiyo haitakuwa na maana na haiwezi kutupa maendeleo kama hatuna usalama kama hayuna utulivu "
Amesema kuwa katika kukusanya maoni ya dira ya Taifa swala la amani linapaswa kuzingatiwa kwani bila amani , Utulivu na usalama, dira haiwezi kufanya kazi .
Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu Tawala wa wilaya zote, wakuu wa idara, wakuu wa Taasisi, viongozi wa dini, wananfunzi, badoboda na wananchi .
Aidha, Mhe Telack amewasisitiza wajumbe wa mkutano huo kuendelea kutoa maoni yao kwa kujaza fomu walizokabidhiwa au kupiga *152*00# na kufuata maelekezo .
Maoni yote yamechukuliwa na timu maalum kutoka Tume ya Mipango kwa hatua nyingine ya ukusanyaji maoni, uchakataji na hatimaye Dira bora ya Maendeleo 2050 kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@maelezonews
Agosti 3, 2024
#dirayataifa2050
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.