Mkuu wa Idara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Bora Haule ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika kikao cha mafunzo ya uwekezaji kupitia Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS kilichofanyika Leo tarehe 13 Juni 2023 kwenye ukumbi wa Ofisi hiyo.
Dkt. Bora amewaasa wafanyakazi kutenga muda wao na kuhakikisha wanafanya shughuli zao za maendeleo ili kuimarisha uchumi wa maisha yao kwa wakati wa sasa na wakati wa kustaafu.
Dkt. Bora amesema kuwa ni vyema kuanza uwekezaji mapema ili kuepuka udanganyifu unaowaingiza wastaafu wengi kwenye dimbwi kubwa la umaskini.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Lindi Una fursa nyingi hivyo wafanyakazi wajitahidi kuzitafuta fursa hizo na kuzitumia ili wawe imara katika kukabiliana na maisha pamoja na changamoto mbali mbali ikiwemo magonjwa.
Aidha, kupitia mafunzo hayo, wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wameelezwa na wataalam kutoka Kampuni ya Uwekezaji ya UTT-AMIS, uwekezaji wa hisa kwenye kampuni kupitia UTT inamuwezesha kila mmoja hasa wenye vipato vidogo kushiriki na Kukuza mtaji wake.
Pia Uwekezaji kupitia UTT inamrahisishia muwekezaji kazi ya kutafuta sehemu ya kuwekeza yenye usalama na uhakika wa Kukuza mtaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.