Naibu Katibu Mkuu upande wa Afya kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Wilson Mahera Leo Jumatano amezindua mafunzo ya mfumo Mshitiri utakaotumiwa na vituo vya huduma za afya kufanya manunuzi ya madawa.
Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Mahera ameeleza kuwa mfumo Mshitiri upo na umekuwa ukitumika muda mrefu lakini haukua mfumo wa kielekroniki. Hivyo uzinduzi huu unafanyika kwa ajili ya mfumo wa Mshitiri ukioboreshwa ambao unafanya kazi kielekroniki.
Dkt. Mahera ameongeza kuwa kwa kutumia mfumo huu utasaidia upatikanaji wa dawa na udhibiti changamoto za taratibu za ununuzi wa dawa. Mfumo huu unaweka wazi taratibu pamoja na bei za ununuzi wa dawa hivyo ni vigumu kufanya udanganyifu.
Awali akizungumza mbele ya wajumbe wa mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Khery Kagya amesema kuwa Serikali imeleta mfumo huu ili kurahisisha upatikanaji wa wazabuni wa kusambaza dawa Kwa haraka. Mfumo Mshitiri utaondoa urasimu katika upatikanaji wa dawa. Ameongeza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi ilikuwa asilimia 88.6 Kwa mwaka 2021/22, na Kwa mwaka huu 2022/23 upatikanaji wa dawa ni asilimia 91.5.
Mafunzo ya Mfumo Mshitiri yatafanyika Mkoani Lindi katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Sokoine ikiwahusisha Waganga Wakuu wa Wilaya, Wataalam wa afya, Wataalam wa TEHAMA, Maafisa Habari pamoja na Maafisa manunuzi kutoka Halmashauri na Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.