Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewaomba wakazi wa Mkoa wa Lindi kujitokeza kumpokea na kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt SAMIA SULUHU HASSAN wakati wa ziara yake katika mkoa wa Lindi anayotarajiwa kuifanya kuanzia Septemba 17 hadi 19, 2023. katika maeneo ambayo atapita sambamba na kuhudhuria katika mikutano ya hadhara.
Mhe.Telack amesema akiwa Mkoani Lindi Mhe. Rais anatarajiwa kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali pamoja na kuongea na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Mapokezi ya Dkt. Samia Suluhu Hassani yatafanyika katika wilaya ya Liwale kisha kuelekea Nachingwea ambapo atatembelea kuona chumba kipya cha Kisasa cha wagonjwa mahututi kilichofungwa vifaa vya kisasa(ICU) na baadae kufanya mkutano mkubwa katika uwanja wa Malori Nachingwea.
Maeneo Mengineyo ni Wilaya ya Ruangwa ambapo Mhe. Rais anatarajiwa kuongea na wananchi kupitia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kilimahewa na kufuatiwa na uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara Nanganga- Ruangwa Km 53.5 inayojengwa kwa Kiwango cha lami.
Katika Halmashauri ya wilaya ya Mtama ataweka jiwe la Msingi katika jengo jipya la halmashauri hiyo, Kilwa ataweka jiwe la Msingi ujenzi wa bandari ya uvuvi na Lindi Manispaa Rais anatarajiwa kuweka Jiwe la msingi katika shule mpya ya sayansi ya wasichana Kilangala na kisha kufuatiwa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hospitali Mpya ya rufaa ya Mkoa wa Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.