Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack ametoa pongezi hizo Jana Alhamisi katika kikao cha Idara ya elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Kikao hicho kilichojumuisha wadau mbalimbali kulikuwa na lengo la kuwasilisha mpango mkakati wa Mkoa unaolenga kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa mwaka 2023.
Pamoja na pongezi hizo , Mhe. Telack amesema kuwa Mkoa wa Lindi Kwa ujumla umefanya vzuri Sana kwenye matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka mwaka huu, hivyo kuna haja sasa ya kuboresha mazingira ya walimu.
"Nitumie nafasi hii kuwapongeza walimu wanafunzi na wazazi wote kwa kazi nzuri na kubwa walioifanya.........ki ujumla matokeo ya kidato cha nne mkoa wetu umefanya vizuri sana". Amesema Mhe. Telack.
Mhe. Telack ametoa wito kwa wazazi na wadau kuunga mkono jitihada za walimu kwa kuboresha mazingira yao ya kufundishia pamoja na makazi. Amesisitiza kuwa wadau waunganishe nguvu kwa pamoja ili zijengwe nyumba za walimu na kuwapa nafasi ya kufanya kazi yao kwa utulivu. Pia amezitaka Halmashauri kutumia mapato ya ndani kujenga nyumba za walimu ili wautumie muda wao wa kazi vizuri.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Ngusa Samike wakati akifungua kikao cha Maabara ya elimu kilichofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu, Nachingwea amewataka walimu kuwafuatilia wanafunzi wanaoacha shule na kuingia mtaani na kujiingiza kwenye ajira za utotoni.
Ndg. Ngusa Ameongeza kuwa walimu wanatakiwa kuwasimamia watoto toka wanapoandikishwa darasa la awali na kuwafuatilia mpaka wanapohitimu shule kwa ngazi zote.
Amewataka walimu wote kubuni mikakati madhubuti itakayowavutia na kuwahamasisha wanafunzi kuendelea na masomo ili baadae Taifa liwe na wasomi wa kutosha.
Kwa upande wake, Afisa elimu Mkoa wa Lindi Ndg. Joseph Mabeyo amesema kuwa Mkoa unaendelea kushirikiana na wadau wote wa elimu ili kufikia malengo yaliyowekwa. Mkoa unaendelea kutekeleza na kubuni mikakati itakayotokomeza matokeo ya daraja sifuri kwa watahiniwa wa kidato cha nne.
Ndg. Mabeyo ameongeza kuwa idadi ya watahiniwa waliopata daraja sifuri kwa mwaka 2021 walikuwa 539 na mpaka kufikia mwaka 2022 idadi hiyo ilipungua na kufikia 334.
Jitihada za Walimu katika kuleta mapinduzi ya elimu kwa Mkoa wa Lindi zinaendelea kuzaa matunda mazuri ambapo Kwa mujibu wa taarifa za Baraza la Taifa la Mitihani za mwaka 2019-2020, Mkoa wa Lindi umetajwa kuwa Mkoa pekee uliopandisha kiwango cha ufaulu kwa miaka mitatu mfululizo.
ReplyForward |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.