Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Majid Myao amewaasa wananchi kuwekeza katika kilimo cha mazao ya muda mrefu hasa miti ya biashara.
Ndg. Myao amesema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika jana jumatano tarehe 20 Machi 2024 katika jengo jipya la Ofisi za Halmashauri ya Mtama linaloendelea kujengwa, eneo la malengo B.
Amesema kuwa Kwa kipindi kirefu jamii ya Mkoa wa Lindi imekuwa ikijihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali kama vile Korosho, ufuta, mahindi miti ya mikorosho, mbaazi ambayo Kwa kiasi kikubwa ni mazao ya muda mfupi.
Ameongeza kuwa sasa imefika wakati wa kuwekeza katika kilimo cha miti ambacho kimewainua kiuchumi wananchi wengi wa maeneo mengine nje ya Mkoa wa Lindi.
Amesisitiza kuwa pamoja na kilimo cha mazao ya muda mfupi ni vyema kubadili tabia na kuanza kufanya uwekezaji wa mazao ya muda mrefu ambao husaidia kuimarisha uchumi wa mmoja mmoja na familia na kupunguza kadhia mbalimbali hasa katika kipindi cha uzeeni.
Leo jumatano tarehe 20 Machi 2024, kupitia uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkoa wa Lindi umepanda jumla ya miti 400 kuzunguka eneo la jengo jipya la Ofisi ya Mtama huku wananchi wakipatiwa miche ya miti aina ya mitiki Kwa ajili ya kupanda kwenye maeneo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.