TAASISI ya Young Scientists (YST) imewatangaza wanafunzi wa Shule za Sekondari Tatu kuwa washindi wa Maonesho ya wanasayansi chipukizi ngazi ya Mkoa wa Lindi.
YST imesema wanafunzi hao wameibuka washindi baada ya kubuni miradi mbalimbali ambayo imekuwa ya kipekee na kuonekana na tija katika jamii.
Washindi wa kwanza katika Maonesho hayo ni wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Kibutuka ambayo ipo Wilaya ya Liwale ambao ni Afidhi Maulidi Kilete na Oktoba Chande Makanwa.
Wanafunzi hao wameibuka washindi baada ya kubuni mradi wa dawa ya asili ya Meno na kinga yake. (Natural Toothpaste and its Treatment).
Nafasi ya pili imeshikwa na Yasari Yasini Ndutuli na Fakihi Ibrahimu Athumani kutoka shule ya Sekondari Nachingwea iliyopo Wilayani Nachingwea. Wao wameshika nafasi hiyo baada kuandaa mradi wa Dawa ya kupambana na wadudu na magonjwa katika mimea (Power of the Mixture of Wood Ash, Soap, Red Peppers and Sunflowers for Fighting Pests and Diseases in Plants)
Na nafasi ya Tatu imeshikwa na Mariamu Rashid Mussa na Ernest Antony Matamilili kutoka Shule ya Sekondari Angaza iliyopo Manispaa ya Lindi.
Wanafunzi hao wa Angaza Sekondari wameandaa mradi wa kutumia maji taka yanayotokana na matumizi ya nyumbani kufanya umwagiliaji wa mazao mbalimbali (Use of Domestic Waste Water for Irrigation of Vegetables Crops).
Shule hizo tatau kutoka amKoa wa Lindi zimepata medali na kupata fursa ya kushiriki mashindano ya kitaifa Jijini Dare Es Salaam.
Akizungumza katika maonesho hayo yaliyofanyika katika ukumbui wa shule ya Sekondari WAMA iiliyopo Manispaa ya Lindi, Mkurugenzi wa YST Dk Gozberth Kamugisha amesema washindi hao wanapata Medali, fedha na fursa ya kushiriki Maonesho ya Kitaifa Jijijini Dar Es Salaam ambako wakishinda watashiriki maonesho ya kimataifa ya wanasayansi Chipukizi.
Wilaya zote kutoka Mkoa wa Lindi zimeshiriki mafunzo hayo na Shule sita zimepata zawadi ya Medali.
Dr Kheri Mwijage Kagya amewashukuru sana YST kwa kuuchagua Mkoa wa Lindi kushiriki Maonesho hayo ya wanasayansi Chipukizi, kwani inatoa hamasa kwa wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi na kuongeza ufaulu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.