Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa wameipongeza Shule ya Lindi Sekondari kwa maendeleo makubwa kwenye ufaulu wa wanafunzi hasa kidato cha sita.
Pongezi hizo wamezitoa jana alhamisi walipoitembelea Shule hiyo Kwa ajili ya ukaguzi wa fedha zilizotolewa na Serikali kwa lengo la ukarabati na ujenzi wa madarasa mapya.
Akitoa pongezi hizo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Halima Mdee (Mbunge) amesema anaipongeza Shule na Walimu wote kwa kuutoa Mkoa wa Lindi kutoka mikoa ambayo ilikuwa haiheshimiki kwenye maendeleo ya elimu hapa nchini.
Mhe. Mdee ameongeza kuwa kwa mabadiliko haya makubwa ya elimu, mikakati iliyowekwa iendelezwe na kuendelea kuwapa nguvu zaidi Walimu ili wajitume zaidi.
Awali akisoma taarifa ya Shule hiyo, Mkuu wa Shule Mwalimu Ramadhani Abdallah Divelle amesema kuwa Shule ya Lindi Sekondari kwa kidato cha sita ndani ya miaka mitatu mfululizo hali ya taaluma kwa kipindi hicho imefanya vizuri Sana.
Kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2020 Shule ilikuwa na jumla ya watahiniwa 204 Kati ya hao watahiniwa 27 walifaulu kwa daraja la kwanza, watahiniwa 130 walifaulu kwa daraja la Pili, watahiniwa 44 walifaulu kwa daraja la nne na watahiniwa 3 walifaulu kwa daraja la nne, ufaulu huu ukiwa ni asilimia 100.
Mwaka 2021, jumla ya watahiniwa walikuwa 173 na Kati ya hao 93 walifaulu kwa daraja la kwanza, 53 daraja la Pili, 27 daraja la tatu, ikiwa ni ufaulu wa asilimia 100.
Mwaka 2022 Shule ilikuwa na watahiniwa 232 na Kati ya hao 116 walifaulu kwa daraja la kwanza, 105 walifaulu kwa daraja la Pili na 11 walifaulu kwa daraja la tatu, ikiwa ni ufaulu wa asilimia 100.
Akizungumza kama muhasisi wa mabadiliko hayo makubwa ya elimu Mkoani Lindi, Mkurugenzi wa Elimu kutoka OR-TAMISEMI Ndg. Vicent Kayombo amesema kuwa kabla ya kuwa mkurugenzi alikuwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Lindi.
Ndg. Kayombo ameeleza kuwa akiwa Afisa Elimu wa Mkoa aliimarisha uongozi Bora na imara kwenye sekta ya elimu, kujenga upendo kwa Walimu na kushughulikia changamoto zao, kutoa motisha kwa Walimu pamoja, ku na kuandaa mpango wa Elimu wa Mkoa. Na Nchi nzima Mkoa wa Lindi pekee ulikuwa mpangokazi wa uboreshaji elimu.
Historia ya elimu ya Mkoa wa Lindi kwa miaka mingi imekuwa si ya kuridhisha. Ufaulu wa watahiniwa kwa Shule zote za msingi na Sekondari ulikuwa wa kiwango cha chini. Jitihada zilizofanywa na Viongozi wote wa Mkoa zimezaa matunda Bora ambayo yameufanya Mkoa wa Lindi kushika nafasi za kwanza na pili kwenye matokeo ya kitaifa ya kidato cha sita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.