Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali ya Mitaa Leo Jumanne imeagiza kuongeza idadi ya wafanyakazi ili kumaliza mradi wa ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Mtama Kwa wakati uliopangwa.
Maelekezo hayo yametolewa na Kamati hiyo Leo Jumatano ilipotembelea ujenzi wa mradi wa Ofisi hiyo unaotekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT kanda ya Kusini.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo, Viongozi kutoka OR- TAMISEMI, Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Viongozi wengine, Menyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Halima Mdee (Mbunge) amewataka SUMA JKT kuongeza nguvu kwenye mradi huo ikiwemo kuongeza wafanyakazi ili kuongeza Kasi ya ujenzi wa mradi. Mhe. Mdee ameongeza kuwa muda alioongezewa mkandarasi kumaliza mradi umebaki mchache hivyo anapaswa kutumia nguvu ya ziada ili kuendana na muda.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa Mkandarasi SUMA JKT anaejenga mradi huo kufanya kazi Kwa mujibu wa makubaliano na kuhakikisha unamalizika kwa wakati uliopangwa.
Aidha, Msimamizi wa ujenzi wa mradi huo, Kop. Laurent Marwa ameleeza kuwa kuchelewa kwa mradi huo ulitokana na Halmashauri kubadilisha mchoro wa ramani pamoja na mvua. Kop . Laurent Marwa ameongeza kuwa mpaka kufikia mwezi Julia 2023, ujenzi wa mradi utakuwa umekamilika kwa asilimia 100 kama ilivyopangwa.
Mradi huu wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mtama unajengwa na Mkandarasi SUMA JKT kwa thamani ya Bilioni 3.7 ambapo mpaka Kamati ya Kudumu ya Bunge inautembelea umefikia umefikia asilimia 60 na mwezi Julai 2023 unatakiwa umalizike.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.