Kayombo: Maandalizi ya mtihani wa taifa wa darasa la saba 2019 yakamilika mkoani Lindi.
Afisa elimu wa mkoa wa Lindi, Ndg. Vicent Kayombo amehakikisha kukamilika kwa maandalizi ya mitihani ya taifa wa darasa la saba inayotarajiwa kuanza kesho Septemba 11, 2019 nchi nzima.
Katika maelezo yake Ndg. Kayombo amesema mkoa umejipanga vizuri kuendesha mitiani hiyo, ambapo baada ya kupokea maelekezo maelekezo kutoka baraza la mitihani la taifa mkoa ulichukua hatua zote muhimu kuhakikisha mitiani hiyo inafanyika vizuri bila tatizo lolote. Pia kamati ya mitihani mkoa imejipanga na kutoa maelekezo kwa kamati zote za kata, wilaya na halmashauri za mkoa kuhakikisha mitiani hiyo inafanyika kiusalama.
Aidha, ameeleza jitihada mbalimbali zilizofanywa na mkoa katika kuwaandaa watahiniwa ili kuongeza ufaulu kuwa ni pamoja na kuwa na vituo vya mada ngumu katika kata zote ndani ya mkoa ambapo watahiniwa waleweza kukusanywa pamoja na kufundishwa. Pia kupitia vipimo mbalimbali vya mitiani kama Mock wilaya na Mock mkoa na baadae mkoa uliendesha mtiani maalum wa Pre-National mwezi Julai miezi miwili kabla ya mtiani wa Taifa na kupata ufaulu wa 86.1%. Hivyo mkoa ulipata miezi miwili ya ziada kufanya marekebisho kwenye madhaifu na makosa mbalimbali yaliyoonekana kwa watahiniwa wetu.
Kadhalika na hayo ndg. Kayombo ametoa pongezi kwa walimu na wazazi kwa kuonyesha ushirikiano katika kipindi chote cha maandalizi ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo mbalimbali na kuhakikisha uwepo wa chakula katika vituo vyote vya madangumu na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo katika kipindi hiki cha mitihani.
“Niwaombe baadhi ya wazazi kuacha ile tabia ya kuwataka wanafunzi kufanya vibaya kwa makusudi katika mitiani yao kwani serikali kwa sasa inatoa elimu bure lakini pia wapo wafadhili mbalimbali ambao wanajitolea kusomesha wanafunzi wetu”, Alisisitiza Ndg. Kayombo.
Pia,Afisa huyo wa Elimu Lindi amewatakia kila la kheri wasimamizi huo na kuwataka wasimamie kwa kufuata sheria za usimamizi mitiani pamoja na kuwasihi watahiniwa wote kuwahi kufika katika vituo vyao vya mitihani ili kuepuka usumbufu utakaowasababisha kufanya mitiani yao kwa presha. Jumla ya wanafunzi 18,458 wakiwemo wavulana 8,720 na wasichana 9730 wanatarajiwa kufanya mtihani huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.