Kilwa kupiga chapa ng’0mbe 40,000 kwa siku 20
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imejipanga kupiga chapa ng’ombe elfu arubaini katika siku 15 ili kutekeleza agizo la serikali ambalo mwisho wa utekelezaji ni tarehe 31 January, 2018.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa, Ndg. Zablon Bugingo aliyasema hayo mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alipoulizwaa kama halmashauri itaweza kutekeleza agizo hili kwa wakati.
Halmashauri ya Kilwa ilikuwa bado haijaanza kutekeleza agizo la upigaji chapa mifugo kutokana na changamoto ya kifedha lakini walikuwa wanaendelea na utoaji elimu kwa wafugaji juu ya umuhimu wa zoezi hili pamoja na ufugaji bora wa kisasa. Pia halmashauri imeshakamilisha taratibu zote zinazoitajika kwa ajili ukamilishaji wa zoezi hili hivyo halitakwama.
Ndg. Bugingo alisema kuwa halmashauri imeshatoa elimu kwa wataalam 34 wa mifugo ambao kwa sasa wameshapelekwa katika vijiji ambavyo kumewekwa vituo kwa ajili ya upigaji chapa na zoezi hili limeanza leo tarehe 10 Januari, 2018.
“Mhe. Naibu Waziri halmashauri ya Kilwa tumejipanga kuhakikisha kuwa kwa siku hizi zilizobaki tunatekeleza agizo la serikali la upigaji chapa ng’ombe wote elfu arubaini na tutahakikisha mifugo hii haipati madhara yoyote yale wakati wa utekelezaji wa agizo hili”, alisema Ndg. Bugingo.
Katika kukagua utekelezaji wa agizo hili, Mhe. Ulega alitembelea moja ya kituo cha upigaji chapa kilichopo katika eneo la magereza ambapo alikuta zoezi hili likiwa linaendelea na tayari ng’ombe tisini walikuwa wameshapigwa chapa.
Vilevile Mhe. Ulega azungumza na wananchi wa Mji Mdogo wa Kivinje, kijiji cha Matandu na Marendego ambapo katika vijiji vyote hivyo aliwaeleza wananchi juu ya umuhimu wa zoezi la upigaji chapa ng’ombe na kwamba ni zoezi lililopo kisheria. Pia aliwasihi kuendelea kutunza mazingira na kuhakikisha wanapambana na uvuvi haramu ili mazingira ya bahari yaendelee kuwa salama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.