Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa Taifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim amewataka wananchi wa Halmashauri ya Mtama kuitunza miundombinu inayojengwa kwenye maeneo yao.
Ndg. Shaib ameyasema hayo Leo jumanne wakati akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara mita 800 unaotekelezwa na mfuko wa jimbo la Mtama chini ya Mshauri elekezi, Wakala wa Barabara Vijijini, TARURA kupitia Mkandarasi wake SUMA JKT Construction Co. Ltd.
Akizungumza na wananchi wa Mtama, Ndg. Shaib amesema kuwa miundombinu ya barabara inayojengwa inapaswa kutumia na kuitunza ili iwe imara na madhubuti.
"Ndugu Wananchi, tinapaswa kutumia miundombinu hii ya barabara kwa kuitunza na kuifanya iwe imara na madhubuti zaidi, Kwa sababu Barabara hizi zinatuhusu Sisi....hivyo lazima tuthamini fedha yetu ya Tanzania." Amesema kiongozi huyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa barabara kila mwaka kupitia mfuko wa jimbo la Mtama.
Mhe. Nape ameongeza kuwa Mhe. Rais anaendelea kutoa fedha Kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Halmashauri ya Mtama ili kuboresha mazingira ya wananchi.
Akieleza maendeleo ya mradi huo mbele ya Mwenge wa Uhuru, Meneja wa TARURA Eng. Dawson Paschal amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo inayotoka Mtama makao makuu kuelekea zinapojengwa Ofisi za Halmashauri ya Mtama kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 52 ambapo gharama halisi za mradi ni Tsh. 499,887,000.00.
Pamoja na mradi huo, Mwenge wa Uhuru imeweka mawe ya msingi katika Miradi 3, umezindua mradi 1, umeona na kutembelea Miradi 8. Mwenge wa Uhuru umeridhika na kuipitisha Miradi yote 12 ya Halmashauri ya Mtama.
Halmashauri ya Mtama imekuwa ya kwanza kuukimbiza Mwenge wa Uhuru baada ya Mkoa wa Lindi kukabidhiwa mapema Leo asubuhi kutoka Mkoa wa Mtwara
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.