Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Leo asubuhi amezindua daraja lililojengwa barabara ya Milola-Nangalu lililojengwa kwa fedha za tozo za mafuta.
Kiongozi wa mbio za Mbio za Mwenge Ndg. Abdalla Shaib Kaim Akizungumza na wananchi pamoja na Viongozi wa Wilaya na Manispaa ya Lindi amewataka Viongozi kusimamia ujenzi wa barabara ya Milola-Nangaru ikamilike mapema ili wananchi wanufaike na miundombinu inayojengwa na Serikali yao.
Akimshukuru kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kwa kufika Jimbo la mchinga, Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Salma Kikwete amesema kuwa kazi kubwa ya Mwenge wa Uhuru ni kuimulika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali.
Mhe. Salma Kikwete ameeleza adha waliokuwa wanaipata wananchi wa Kata ya Milola na Nangalu Kwa kukosa Mawasiliano kwa zaidi ya miaka 15. Ameongeza kuwa kufunguka kwa Mawasiliano Kati ya Kata hizo kutafungua fursa mbalimbali na kuongeza uchumi wa wananchi wa Pande zote mbili na maeneo mengine jirani.
Mhe. Salma Kikwete ameongeza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kulipatia Jimbo la Mchinga fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambazo zimesaidia kutatua changamoto nyingi za wananchi.
Akisoma taarifa ya mradi wa daraja hilo, Meneja wa TARURA Vijijini Eng. Dawson Paschal amesema kuwa ujenzi wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 tangu tarehe 09 Desemba 2022 huku ukigharimu kiasi cha fedha jumla ya Tsh. 778,665,000.00.
Eng. Dawson ameongeza kuwa kukamilika kwa daraja hilo na barabara kutawawezesha wananchi kusafirisha mazao ya na bidhaa za Biashara kirahisi na kuokoa muda.
Pamoja na kukamilisha ujenzi wa daraja hilo, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini,TARURA wanaendelea na ujenzi wa barabara ya Milola - Nangalu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.