Hayo yamesemwa jana tarehe 31 Mei 2023 na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dr. Steven L Kiruswa(Mb) alipomuwakilisha mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufunga kongamano la Chama cha Wanawake Wachimba Madini Mkoani Lindi.
Mhe. Kiruswa Akizungumza na wanawake wanaojishughulisha na shughuli za madini pamoja na fursa zingine zinazozalishwa na sekta ya madini katika ukumbi wa ghalani katika Wilaya ya Ruangwa, amesema kuwa kiwanda cha kuchakata chumvi kitajengwa Mkoani Lindi.
Mhe. Kiruswa ameeleza kuwa, Serikali ililielekeza Shirika la Madini la Taifa kuwekeza kiwanda cha kuchakata chumvi ambacho kitahudumia wazalishaji wa bidhaa hiyo kwa mikoa ya pwani, Lindi na Mtwara.
Ameongeza kuwa Uwekezaji wa kiwanda hicho unalenga kutatua changamoto ya soko la chumvi ghafi ambayo imekuwa ikiwaadhiri kwa muda mrefu wakulima wa bidhaa hiyo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amemueleza Naibu Waziri kuwa wananchi wanajitahidi kutumia fursa za Mkoa wa Lindi Kwa kiasi kikubwa lakini jitihada zao zimekuwa zikirudishwa nyuma na changamoto ya masoko.
Mhe. Telack amesema kuwa soko la madini ya Jasi pamoja na chumvi limekuwa halipatikani baada ya wanunuzi wa mali ghafi hizo kuagiza nje ya nchi. Ameongeza kuwa Kampuni ya Nill Salt iliyokuwa ikinunua chumvi kutoka kwa wakulima wa Lindi ni muda mrefu ameacha na inasemekana kwa sasa anaagiza chumvi kutoka nje.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Lindi, Bi. Palina Ninje kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Lindi wanaojishughulisha na uchimbaji Madini amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua Lindi kiuchumi hususani kupitia sekta ya madini.
Bi. Palina amesema kuwa lengo la kufanya kongamano la wanawake wachimba madini ni kuwafungua macho wanawake wa Mkoa wa Lindi kuziona fursa zilizopo kwenye sekta ya madini na kuweza kuzichangamkia.
Kongamano hilo limefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 30-31 Mei 2023 katika ukumbi wa ghalani uliopo Wilaya ya Ruangwa likijumuisha wanawake kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Lindi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.