Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, TFRA Dkt. Antony Dialo amewataka wananchi wa Lindi kujiandaa na mabadiliko ya kiuchumi yanayotarajiwa kuibuka Mkoani Lindi miaka michache ijayo.
Dkt. Dialo ameyasema hayo jana jumatatu katika kikao cha tathmini ya mfumo mzima wa upatikanaji wa mbolea ya ruzuku inayotolewa na Serikali kwa wakulima wa Mkoa wa Lindi kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kupitia kikao hicho amewasihi wananchi wa Lindi kuwa, pamoja na ukuaji wa Shughuli zingine za maendeleo kama vile viwanda na biashara, wakulima wasiiache fursa ya kilimo na badala yake waongeze nguvu ya kuzalisha bidhaa za kilimo.
Dkt. Dialo ameongeza kuwa Mkoa wa Lindi una ardhi bora na mabonde mazuri kwa maendeleo ya kilimo, hivyo wakulima wa Lindi wasipotumia fursa hizo ipasavyo, bidhaa nyingi za chakula zitatoka kwa wakulima wa mikoa mingine.
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea nchini, TFRA imekutana na wadau wa mbolea na kuzungumza nao jana tarehe 23 Oktoba 2023 baada ya kufanya ziara Mkoani Lindi kujionea hali ya upatikanaji na matumizi ya mbolea kwa wakulima wa Lindi.
ReplyForward |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.