Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Bi. Zainab Telack amezindua rasmi maadhimisho ya siku ya Mwalimu wa darasa la kwanza mkoa wa Lindi ikiwa ni njia ya kutambua na kuthamini mchango unaofanywa na walimu hao katika kujenga msingi bora wa kitaaluma kwa wanafunzi kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu .
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa ameitaka jamii na walimu kusimama kuirudisha heshima na hadhi ya ualimu ambapo amesema “Tunataka heshima ya mwalimu irudi, na sisi walimu tusimamie kurudisha heshima ya ualimu, na ndio maana Hayati baba wa Taifa, mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki akiwa anaitwa mwalimu kwakuwa alitambua heshima na thamani ya mwalimu’’
Aidha, kwa kutambua mchango wa walimu kwa maendeleo ya sekta ya Elimu ndani ya mkoa wa Lindi, Mkuu wa mkoa amesema kuwa mkoa umedhamiria kutumia mapato ya ndani ya halmashauri kujenga nyumba za walimu ili kuwawezesha kupata sehemu nzuri za kuishi na kuongeza kuwa ushirikiano baina ya wazazi na walimu ni muhimu katika kusimamia maendeleo ya mwanafunzi.
Katika maadhimisho hayo yaliyokua na kauli mbiu ya ‘Mwalimu wa darasa la kwanza, msingi wa taaluma yangu’, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Dokta. Bora Haule amesema kuwa mkoa umeamua kuadhimisha siku hii kila ifikapo tarehe 24 Novemba ili kutambua umuhimu wa walimu wa darasa la kwanza wanapowasilisha matatizo yao,kuwapa hamasa na kuwafanya wajione sawa na walimu wa madarasa mengine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.