Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary akizungumza katika kikao cha baraza la Chama Cha Walimu Mkoa wa Lindi, amesema kuwa licha ya Serikali kuendelea kulipa na kutoa stahiki za watumishi wakiwemo walimu , serikali imeiletea fedha nyingi Mkoa wa Lindi kwaajili ya miundombinu mbalimbali ya elimu , kiasi cha Bil 23.
Fedha hizo zinamchanganuo ufuatao, Bil 4.3 za Boost zitajenga shule mpya 7 za msingi , ukarabati wa shule 5 za msingi, Matundu ya Choo 114 na madarasa 54, Fedha Bil 16.07 za SEQUIP zitajenga Shule 1 ya wavulana ya kanda, shule za kata 6 , Shule ya Amali Mkoa 1, Shule 7 za Amali Wilaya, Nyumba za walimu 9, Madarasa 18, , Mabweni 11, Vyoo 52, fedha za EP4R Bil 2.1 zitamalaizia Mabweni 13 na kujenga mabweni mapya 12 na Milioni 806 za BARRICK zitajenga madarasa 11, Mabweni 4 na vyoo 18.Sambambao na fedha hizo Bi. Zuwena ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wasimamizi wote wa fedha hizo kuzingatia matumizi sahihi kwa mujibu wa utaratibu na muongozo bila kusahau ushirikishaji wa jamii katika utekelezaji wa mradi katika eneo husika.Aidha, ameshukuru uongozi wa CWT Mkoa kwa mwaliko wao na wasilisho la changamoto za walimu, amewasihii kuendelea kuwa nasubira kwani serikali ya awamu ya sita inaendelea kuchukua hatua za makusudi kumaliza changamoto hiyo " kwa mwaka huu pekee fedha zaidi ya bil 1.19 zimelipa madeni mbalimbali ya watumishi wa Mkoa wa Lindi " Katibu Tawala alieleza.Kwa upande wake katibu wa chama cha walimu Mkoa wa Lindi Bi. Sekela Msagala amemshukuru sana mgeni rasmi kwa kuitikia wito na kupokea changamoto za walimu kama vile madai ya watumishi yakiwemo fedha za uhamisho na Likizo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.