Madaktari Bingwa na Ubingwa Bobezi wa Rais Samia wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa mwanaume mwenye umri wa miaka (41) Mkazi wa Wilaya ya Nachingwea na kufanikiwa kuziba Mfuko wake wa chakula uliokuwa na matundu mengi.
Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea Dkt. Shukrani Nsikini leo Septemba 19,2024 na kusema kuwa upasuaji huo umefanyika Septemba 18,2024 katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea ukiongozwa na Daktari Bingwa Norbet Njee kutoka hospitali wa Kanda ya Ligula-Mtwara akishirikiana na Dkt. Rajab Sadiki wa Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.
“Tulipata mgonjwa mwanaume ambaye alikuwa anaeleza kuwa anaumwa tumbo na anakosa choo, lakini baadae akawa anapata choo kidogo na maumivu makali yaliyopelekea tumbo kuvimba, Daktari bingwa alipo muangalia akasema mgonjwa anahitaji upasuaji.” Amesema Dkt. Nsikini.
Dkt. Nsikini ameendelea kueleza kuwa baada ya kumfanyia upasuaji waligundua kwamba Mfuko wa chakula ulikuwa na matundu mengi na kupelekea chakula kuvujia tumboni na kusababisha mgonjwa kukosa nguvu kabisa.
“Alikuja hapa akiwa amedhoofu sana hatujawahi kupata mgonjwa wa aina hii na kuruhusu kumfanyia upasuaji lakini Dkt. Njee alisema tunamfanyia na atakuwa salama, mfuko wake wa chakula ulikuwa una matundu mengi na hivyo chakula kushindwa kuendelea kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa kawaida.” Amesema Dkt. Nsikini
Dkt. Nsikini amesema upasuaji umekuwa wa mafanikio na mgonjwa ameamka na sasa anaendeelea na mazoezi madogomadogo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.