Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amefungua mafunzo yaliyotolewa kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Lindi mwishoni mwa mwezi Aprili 2024.
Mafunzo hayo yametolewa na wawezeshaji kutoka Sekta ya Afya, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, TAKUKURU, Haki Jinai, Sekretariet ya Maadili ya Utumishi wa Umma Kanda ya Kusini, Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika ukumbi wa mikutano wa Double M Hoteli iliyopo Manispaa ya Lindi.
Aidha, Maafisa wa Jeshi la Polisi wamepatiwa mafunzo ili kuimarisha utendaji wa jeshi hilo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na kuimarisha utendaji, pia Maafisa hao walielezwa kuhusiana na fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo Mkoa wa Lindi ambazo wakiweza kuzitumia vizuri zitaimarisha uchumi wao katika kipindi cha kazi na hata maisha ya kustaafu.
Mafunzo hayo pia yalihudhuliwa na Kamishna wa Utawala na Menejimenti Rasilimali Watu Jeshi la Polisi Tanzania CP Suzan Kaganda pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi ACP John Imori.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.