SERIKALI YAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MBOLEA KWA WAKULIMA.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Udhibiti Mbolea, TFRA imeendelea kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa mbolea kwa wakulima wa nchi nzima ikiwemo Mkoa wa Lindi.
Hayo yamebainika kupitia kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa TFRA na wadau wa mbolea wa Lindi kilichofanyika jumatatu ya tarehe 23 Oktoba 2023 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Katika kikao hicho, changamoto kubwa iliyojitokeza ni elimu kwa wadau wa mbolea hasa wakulima kuhusiana na uelewa na matumizi ya Mfumo wa ruzuku ya Mbolea ambo unatumika kusajili wakulima na mahitaji yao ya mbolea.
Aidha, wataalam wa kilimo wameelekezwa kuwasaidia wakulima kwa kuwapatia elimu ya matumizi sahihi ya mfumo huo ili waweze kupata mbolea mapema katika kipindi hiki cha maandalizi ya kilimo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.