Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt.Seleman Jafo akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ametoa pongezi kwa viongozi na wakulima kwa utekelezaji mzuri wa utaratibu wa matumizi sahihi ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kusisitiza umuhimu wa mfumo huo, katika kuhakikisha uwazi na ufanisi wa masoko ya mazao.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa muendelezo wa ziara maalumu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo na kuhimiza juu ya matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa ni nguzo muhimu katika kudhibiti ubora wa mazao na kuhakikisha uaminifu katika biashara.
"Mfumo wa stakabadhi ghalani ni lazima utekelezwe kwa ufanisi, ili kuwalinda wakulima, kuwawezesha kupata bei stahiki, na kuhakikisha wateja wanapata kiasi kamili cha mazao wanachonunua, bila upungufu, na niwambieni huu ndio mkombozi wa wakulima na njia pekee ya kuimarisha ushindani wa mazao yetu, katika masoko ya ndani na nje ya nchi".Dkt.Jafo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.