Leo tarehe 18 Julai 2022 akizungumza Wilayani Ruangwa Waziri wa Afya , Mhe. Ummy Mwalimu ametangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa mpya wilayani humo kuwa ni homa ya Mgunda. Ugonjwa huo husabisha utokwaji wa damu puani, kuishiwa nguvu na hata kupoteza maisha.
Homa ya mgunda husababishwa na wanyama hasa panya, swala na mbweha ambao wanapatikana ukanda mzima wa kusini. Maambukizi ya ugongwa huu hutokana na mkojo wa wanyama hao hasa kwenye vyanzo vya maji vinavyotumiwa na jamii, pia kugusa udongo, vyakula vilivyochafuliwa na wanyama hao.
Tangu kuripotiwa kwa ugongwa huo Julai 13,2022 jumla ya wananchi 20 wameugua homa ya mgunda Wilayani Ruangwa ambapo watatu kati ya hao wamekwisha poteza maisha.
Hata hivyo, tayari dawa ya ugonjwa huo imepatikana na namna ya kujikinga Kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali pamoja na wadau wengine kupitia timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya dharura na majanga,Epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Utafiti (NIMR), Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.