#matukiokwapicha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack akizungumza na Mwenyekiti wa Muda wa ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi Ndugu Seleman Bungara, wilayani Kilwa..
Bungara aliomba kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa lengo la kujitambulisha na kukabidhi taarifa ya mpango kazi wake kama kiongozi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi.
Mhe. Telack amepokea taarifa hiyo mara baada ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari ya kilwa na utatuzi wa mgogoro wa ardhi, amemsihii kuwasisitiza wananchi kulima mazao ya chakula kama ambavyo Serikali imekuwa ikisisitiza.
Picha Ndugu Seleman Bungara akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack
Mhe. Telack amepongeza hatua na kasi ya ujenzi wa mradi wa bandari ya uvuvi ya kisasa , amekabidhi baiskeri mbili kwa watu wenye mahitaji maalumu na ametatua mgogoro wa ardhi kati ya familia na mwekezaji ambao umedumu kwa muda wa zaidi ya miaka 10 .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.