Mhe. Magufuli atoa zawadi za sikukuu katika Kituo cha Walemavu Nandanga.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli ametoa zawadi kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka katika Kituo cha Walemavu wa Ukoma Nandanga.
Kituo hichi cha ukoma Nandanga kipo katika Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na kilianzishwa mwaka 1973. Mpaka sasa kituo kina jumla ya walemavu 31 ambapo kati yao wapo walemavu wawili wa Mtindio wa Ubongo na wawili ni walemavu wa ngozi wote wakiwa ni wanawake.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe. Rais, Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Ndg. Ramadhani Kaswa aliwaeleza kuwa Mhe. Magufuli kama ilivyo desturi yake ametoa zawadi kwenye Kituo cha Nandanga kwa ajili ya sikukuu hii ya Pasaka ili kila mmoja aweze kusheherekea. Zawadi hizo ni mchele kilo 100, mbuzi mmoja na mafuta ya kupikia lita 10.
Ndg. Kaswa aliwaeleza kuwa Mhe. Magufuli amewatakia heri na sikukuu njema ya pasaka na kuwa serikali inawatambua na itaendelea kuwa pamoja nao.
Akishikuru kwa zawadi hizo, Mwenyekiti wa Walemavu, Ndg. Shaibu Mohamed Mtai alisema kuwa wanashukuru sana huku akimuomba Ndg. Kaswa kuhakikisha anazifikisha shukrani zao kwa Mhe. Rais. Pia alimshukuru Ndg. Kaswa na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya kwa kuzifikisha zawadi pamoja na ushirikiano wanaowapa katika kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.