Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika kongamano la kisayansi lililofanyika jana Mkoani Lindi katika Ukumbi wa Hoteli ya Sea View likiwa na lengo kuu la kuungana jamii katika kutafakari na kubadilishana mawazo, uzoefu pamoja na mbinu mpya za kisayansi za kupambana na janga la UKIMWI.
Mhe. Katambi amesema kuwa pamoja na mafanikio makubwa tuliyoyapata katika mapambano dhidi ya UKIMWI nchini bado zinahitajika jitihada zaidi kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pamoja na tiba kwa watoto chini ya miaka 5. Ameongeza pia kuwa kundi kubwa la vijana wanapoingia kwenye mahusiano mapya hutumia kinga mwanzo wa mahusiano hayo lakini baada ya muda kupita matumizi ya kinga huwa hayazingatiwi.
Hivyo Mhe. Katambi amewataka wataalam wa kisayansi, watoa huduma na jamii kwa ujumla kuungana kwa pamoja katika mapambano dhini ya UKIMWI kwenye makundi ya jamii ambayo yako nyuma kufikiwa na huduma za VVU na UKIMWI.
Awali akizungumza mbele washiriki wa kongamano hilo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Ndg. Kaspar Mmuya akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana yametokana na jitihada kubwa za asasi za kiraia kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta, hivyo amewataka wadau hao kuendelea kuunganisha nguvu katika mapambano dhidi ya UKIMWI ili kufikia malengo.
Kwa upande wa wadau, Shirika lisilo la Kiserikali la icap ambalo linafanya kazi Mkoa wa Mwanza katika kupambana na UKIMWI kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti wa hali ya maambukizi. Akizungumza kwenye maonesho yanayoendelea katika kiwanja cha Ilulu Mratibu wa Mawasiliano na Uhamasishaji Jamii chini ya icap Bi. Mwanaidi Msangi amesema kuwa utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania hufanyika kila baada ya miaka mitano ambao unasimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, TACAIDS pamoja na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Zanzibar, ZAC, Ofisi ya takwimu Tanzania na Zanzibar, TAMISEMI, Wizara ya Afya pamoja na wadau wengine chini ya ufadhili wa Marekani . Bi. Mwanaidi ameongeza kuwa kwa mwaka 2022/23 utafiti umelenga kuwafikia watu zaidi ya 40,000, kaya 20,000 ambao watapimwa VVU, Homa ya ini B na C.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.