Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack jana alhamisi tarehe 06 Julai 2023 amezindua rasmi Maonesho ya Madini na Uwekezaji.
Mhe. Telack amezindua maonesho hayo kwenye kikao cha wadau wa madini kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mhe. Telack amesema kuwa Maonesho haya yanafanyika maalum Kwa ajili ya kutangaza fursa za madini zilizopo Mkoani Lindi ikiwemo dhahabu yenye ubora wa juu, graphite, gypsum, manganese,nickel, marble, Vito, Safaya na madini mengine isipokuwa Tanzanite na Almasi.
Mhe. Telack ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa fursa za madini, Mkoa wa Lindi una fursa za uwekezaji kwenye kilimo, fukwe nzuri za bahari, utalii, uchakataji wa mazao hasa korosho na ufuta.
Kupitia kikao hicho, Mhe. Telack amewakaribisha wadau wote kwenye sekta ya biashara, Viwanda, madini na sekta zote za uchumi kushiriki kwenye Maonesho ya Madini na Uwekezaji yatakayofanyika Wilayani Ruangwa kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2023.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.