Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewaasa wananchi wa Lindi kumshukuru mungu kwa mvua zinazoendelea kunyesha kwani yeye ndiye aliepanga Kwa sababu maalum.
Mhe. Telack ameyasema hayo katika kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kilichofanyika jana ijumaa tarehe 16 Februari 2024 kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Liwale.
Amesema kuwa mungu ndiye anafahamu sababu ya mvua hizi zinazoendelea kunyesha na hivyo wananchi wanapaswa kumshuru na kutumia fursa hii kwa kupanda mazao kama vile mahindi ya muda mfupi, mbaazi, kunde na mazao mengine ya muda mfupi.
Amewataka wananchi kulima na kupanda mazao hayo lakini pia kupanda aina tofauti tofauti ya mazao mengine ili kujihakikishia mavuno mengi na ya uhakika.
Pia, Mhe. Telack amewaagiza Maafisa kilimo wawatembelee wakulima mashambani na kuwapatia elimu sahihi ya kilimo kwa kipindi hiki cha mvua kilichobaki ili wafanye maamuzi yatakayokuwa na matokeo mazuri.
Hata hivyo, amewaasa wakulima wanaolima mabondeni watafute mashamba mengine kwenye maeneo ya miinuko kwani mvua bado ni nyingi, zinaweza zikaadhiri shughuli za kilimo kwenye maeneo hayo.
ReplyForward Add reaction |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.