Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telackamewaomba viongozi wa dini kuisaidia Serikali kuhamasisha wananchi ili watotowote wapate huduma ya chanjo ya ugongwa hatari wa polio.
Mhe. Telack amewaomba viongozi hao katika kikao cha uzinduzi wakampeni ya chanjo ya ugonjwa wa polio kilichofanyika jana jumatatu tarehe 31Agosti 2022 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Mhe. Telack kupitia kikao hicho amewaondoa wasiwasi wananchi kuwachanjo ya matone ya polio ni salama hivyo jamii iwapeleke watoto kupata hudumahiyo kwenye vituo vya muda vitakavyokuwepo maeneo ya masoko, shule, misikiti,makanisa, mashambani, vituo vya mabasi, maeneo ya Uvuvi na vituo vya kudumu.Lakini pia wataalam wa afya watapita nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kuwapatiawatoto huduma hiyo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Ngusa Samike amesemakuwa serikali imeamua watoto wote chini ya miaka mitano wapatiwe chanjo ilikuwakinga na ugonjwa hatari wa polio ambao umeibuka tena hivi karibuni katika nchi jirani, hivyo zoezi la chanjo litasaidia kuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
Kwa mujibu wa Afisa Afya Ndg. Richard Shabani katika taarifa yakealiyoisoma mbele ya Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ugonjwa wa polio unaenezwa kwakutumia maji au chakula chenye kilichochafuliwa na kinyesi chenye virusi vyaugonjwa wa polio.Hivyo ameongeza kuwa ili kukabiliana na ugongwa huo haina budikuzingatia suala la usafi wa mikono kwa kutumia sabuni na matumizi sahihi yavyoo.
Kampeni ya chanjo ya polio kwa Mkoa wa Lindi ina lengo la kuchanjajumla ya watoto 182,312 ambalo litafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 01Septemba 2022 na kumalizika tarehe 04 Septemba 2022. Aidha, dawa za chanjo hiyozimekwisha sambazwa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi tayari kwautekelezaji. Makundi ya watoto chini ya miaka mitano watakaopatiwa chanjo hiyoni wale ambao walikwisha chanjwa awali na ambao bado hawajawahi kupata chanjo hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.